Friday, January 8, 2016

WAZIRI MKUU AAGANA NA BALOZI WA NAMIBIA

M2

Waziri Mkuu, Kassim Mjaliwa akimkabidhi  Balozi wa Namibia nchini aliyemaliza muda wake, Mhe. Japhet Isaack  zawadi ya ramani ya  Tanzania iliyochongwa kwenye mti wa mpingo  ili aendelee kuikumbuka Tanzania  atakapoondoka. alozi alikwendaofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Januari 8, 2016 kuaga.

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekuaana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Namibia ambaye anamaliza muda wake, Bwana Japhet Isaack.
Akizungumza na Balozi  Isaack leo ,ofisini kwake ,Magogoni jijini Dar es salaa, Waziri Mkuu ameshukuru Balozi huyo na  kumumwomba  waendeleze uhusiano mwema   ulipo baina ya nchi hizi mbili ambao ulianza tangu enzi za kugombania uhuru ili  kusaidia kukuza uchumi wa nchi hizi mbili.
“Namibia ni  nchi yenye uchumi uanaokua haraka, na mmefanikia katika baadhi ya sekta , hivyo ningependa  Tanzania ijufunze kutoka kwenu hasa katika sekta za Utalii, Afya, na Elimu,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
Pia, alitumia fursa hiyo kuwakaribisha  raia wa Namibia kuja kuwekeza nchini  katika maeneo mbalimbali ikiwemo  viwanda  na kuendeleza maeneo ya ukanda maalum ya uwekezaji (EPZ) ili kuongeza thamani ya mazao pamoja na kutatua tatizo la ajira nchini.
Kwa upande wake,  Balozi  Isaack  amesema kwa kipindi alichokaa Tanzania amejifunza mengi, na amefurahishwa  ambavyo Waziri Mkuu pamoja Serikali kwa ujumla  inavyofanyakazi kwa kasi na kwa mafanikio makubwa.
“Hongera, ninafurahishwa na unavyofanya kazi  hongera sana”, alisema Balozi Isack. Pia, amefurahi sana kipindi chote alichokaa Tanzania kwani kimekuwa na matukio mengi yenye kumbukumbu  nzuri kwake.
Balozi Isack   ameomba mahusiano ya nchi hizi mbili yaendelezwe ili zishirikiane zaidi katika masuala mbalimbali ya kukuza uchumi.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P 3021,
11410 DAR ES SALAAM
IJUMAA, JANUARI 8, 2016.

No comments: