ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, August 31, 2011

JK: Kanisa halina mkono Mahakama ya Kadhi

Sheik Mkuu  na musfti Tanzania Issa Bin Shaban Simba akipeana mkono na Rais Dkt Jakaya Kikwete Picha kwa hisani ya MICHUZI
ATAKA MASLHAI YA DINI YAEPUKWE KATIBA MPYA, WAISLAMU WALILIA AMANI AFRIKA
Waadishi Wetu
Rais Jakaya Kikwete amewatetea wakristo nchini kwamba hawahusuiki na kuchelewa kwa mchakato wa kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi, huku akionya kuwa fikra za aina hiyo si za kweli kwani zinaweza kuchochea mgawanyiko kwa misingi ya dini, hivyo kuhatarisha amani nchini.Badala yake Rais Kikwete amesema mchakato wa kuanzishwa kwa mahakama hiyo umecheleweshwa na taratibu ndani ya Serikali na kwamba taratibu hizo zitakapokamilika itaanzishwa na kuendeshwa na Waislamu wenyewe.

Sheik Juma Poli Amir


Sheikh Juma Poli Amir wa Answaar Sunna Tanzania akiongoza ibada ya Eid el Fitr katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam jana. (picha hisani ya blogu ya michuzi)

orijino komedi

Special Airline Fares to and from the U.S

ESM Travel one of the leading travel agency for Tanzanians living in the U.S would like to announce special airline fares to individual and/or groups who will be attending DICOTA Convention from DAR to Washington DC this September. Please call  us at 773-310-9923 or email  travelesm@gmail.com and ask for Elias/Steve Mwita. You can join us on facebook, follow us on twitter and visit us at www.esmtravel.com
Elias Mwita
ESM Travel
2170 S. Goebbert Road Suite 207

DICOTA 2011 CONVENTION $99 VS.$190

Eid Mubarak!
Due to many requests on the Early Bird Registration extension from our main stakeholders, we decided to extend the Early Bird by 1 more week.
The new dates are:


Early Bird Registration fee ends next Wednesday, September 7th 2011 - $99

Late Registration fee starts next Thursday, September 8th 2011 - $190
Last Day to Register is Tuesday, September 20th 2011

Also, as an update, we currently have 215 individuals registered for the convention.
Let's use this extension to get at least another 100 registered by Labor Day!

We are in the midst of announcing the extension:
  • to DICOTA members at large.
  • to TCLA - Tanzania Community Leaders Association, to inform their community members.
  • on our website; counter on DICOTA's website will be updated shortly.
  • through our Facebook account

  • Click Here to Register

bada ya Kiswahili Columbus OH Septemba 4

MISA YA KISWAHILI,WASHINGTON METRO AREA



Watanzania  na wote wanaozungumza lugha ya kiswahili waishio Metropolitan Area(DC,MD,VA)na state za karibu mnakaribishwa katika kushiriki misa ya kiswahili
Lini:9/04/11
Muda:02:30PM(saa nane na nusu mchana)
Wapi:St.Camillus Catholic Church
    
1600 Camillus Dr
    Silver Spring,MD,20903
Kwa maelezo zaidi wasiliana na:
1.Julie Sarwatt-301 648 8232
2.Happiness Marunda-301 461 6030
3.Marco Mbulu-571 426 7124
4.Pius Mutalemwa-301 404 6901
5.Gervas Wambura-301 233 4447
6.Baraka Daudi-301 792 8562
 
Asanteni na karibuni.

Uingereza yapeleka dola bilion 1.6 Libya-BBC

Ndege ya kijeshi ya Uingereza imepeleka pauni milioni 950 Libya baada ya Umoja wa Mataifa kuondoa tanji iliyokuwa imelengwa kwa Kanali Gaddafi.
Noti, zilizotimia dinari za Libya bilioni 1.8 zilizochapishwa Uingereza, zitawasilishwa kwenye benki kuu ya Libya.
Afisa mmoja amesema fedha hizo zinatakiwa ziwepo ili ziingizwe kwenye mashine ya kutolea pesa yaani ATM na kusambazwa kwenye benki haraka iwezekanavyo.
Afisa huyo alisema fedha hizo zitasaidia kulipa wafanyakazi wengi wa sekta ya umma wakati wa likizo ya Eid.
Wengi ambao wanategemea mishahara ya serikali hawajalipwa katika kipindi cha wiki kadhaa.
Hatua hiyo inachukuliwa siku moja kabla ya mkutano mkuu wa kimataifa juu ya hatima ya Libya unaotarajiwa kufanyika mjini Paris siku ya Alhamis.
Mkutano huo utaongozwa kwa pamoja na Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy na waziri mkuu wa Uingereza David Cameron.

Wakazi - Wakati Ndio Huu

Gabon's first lady lived on food stamps in California-ABC News

image.png
The president of Gabon, Ali Ben Bongo, is the son of the country's ruler for the last 42 years and a member of one of the wealthiest families in Africa.

Gabon's new first lady is American-born Inge Bongo. But there'll be no inauguration ceremony or redecorating of the presidential palace for her. Inge Bongo lives in California and is on food stamps.
The new president is confronting angry demonstrations in the streets of the country's capital, Libreville, and other cities protesting what they claim was a rigged election.
The beleaguered president-elect is also facing demands from his estranged wife to be allowed to take her place as first lady and to reform what she says is a lack of human rights.
Inge Bongo makes it clear that she doesn't expect her husband to quickly agree.
"I'm going to claim my right as first lady. I'm going to make a lot of noise. I'm going to take this opportunity to make some changes, whether he likes it or not," Inge Bongo told ABC News. "He can deny a settlement and a divorce. But he's a young man, he's 50. And I'm relatively young. I can just keep doing this forever."
Inge and Ali have had a tempestuous relationship after meeting 23 years ago on a blind date in California. It was love at first sight.

Mkutano Na Muziki Wa Injili Labor Day Weekend

WATANZANIA WAISHIO WASHINGTON  NA MAJIMBO YOTE JIRANI JIRANI MNAKARIBISHWA KATIKA MKUTANO NA MUZIKI WA INJILI JUMAMOSI NA JUMAPILI YA SEPTEMBA 3 NA 4, 2011  

MAHALI
 10110 GREENBELT RD
LANHAM,MD 20706

WAHUBIRI WA KIMATAIFA FRANK CAPORALE,JOHN GRECO, DR NICKU MORDI NA ASKOFU JOSEPH KALEMA WATAHUDUMU PIA WANAMUZIKI MAARUFU WA KIMATAIFA EV. PRINTZE NGOSO, BR. HENRY LUKWAGO NA DADA NANCY MWAMZIMA NA WENGINE WENGI

CHAKULA NA VINYWAJI VITAKUWEPO KWA WOTE

MALAZI KWA WAISHIO MBALI  YATAKUWEPO 

NJOO ILI UPATE MUUJIZA WAKO KATIKA  MKUTANO HUU.

NJOONI WOTE TUMSIFU NA KUMUABUDU MUNGU


MAELEZO PIGA SIMU

APPRECIATION

We would like to take this opportunity to express our sincere appreciation for the support shown to our familiy during this time of grief.
Thanks for the wonderful contributions, the calls, the visits, and prayers. You all have been a big support for late Sebastian Thomas.
Our Lord is merciful and Late Sebastian is at Rest in his Presence.
May God truly bless each of you!
      Everlasting, Bartlet Kamna & Family.
               LOVE YOU ALL!

EID MUBARAK


REMINDER: 1 Day left .....2011 DICOTA....


YOU have only 1 day left to take advantage of $99.00 early registration fee for this year's DICOTA Convention!!!!! It will be $190 from Sept 1st to Sept 20th when doors will be closed.

Few Highlights for this Year's Convention includes (but not limited to):
  • Investments Opportunities and Role of the Diaspora: Learn what role does National Social Security Fund (NSSF), Tanzania Investment Center (TIC), Z'Bar Investment Promotion Agency (ZIPA), Tanzania Revenue Authority (TRA) plays to facilitate engagement and participation in development in Tanzania. Learn how you can utilize Diaspora Desk in our Foreign Affairs & International Cooperation Office.
  • Have a clear understanding on the Role of Central Bank (BOT) and other Commercial Banks in facilitating effective Diaspora Remittances and Providing Capital for Investments. Key figures from BOT, Stanbic Bank Tanzania, CRDB Bank and National Housing Corporation (NHC) to name a few will engage in panel discussion and presentations.
  • USA vs Tanzania Bilateral relations: Familiarize yourself with Millennium Challenge Corporation (MCC) grant and what it has achieved in building Tanzania's infrastructure. 
  • Loan Financing Small and Medium Scale Economic Projects Opportunities for Diaspora?: International Finance Corporation (IFC) World Bank Group will be sending their Country Lead on the subject.
  • Diaspora Access to Land?: The Who Is Who panelist: Mr. Kyando Mchechu-NHC Director General, Dr. Ramadhani Dau-NSSF Director General, Nyumba Poa Ltd Director Mr Peter Malika, to name a few will quest our thirst on the subject. Permanent Secretary Ministry of Land and Housing Development (Ardhi) will present Government plans to assist Diaspora in accessing land in Tanzania.
  • Ever wonder about Employment Opportunities and Challenges for Diaspora Skills Engagement? Radar Recruit CEO will do a presentation on this...and Yes please, BRING YOUR RESUMES!!
  • Do YOU: DICOTA has set aside half a day on Sept 25th for Networking and Job Interviews !
  • Long weekend? How about Maasai BBQ @ the Park, Soccer Bonanza featuring sharp skills from H-Town, TX; Twin Cities, MN; Seattle, WA; City of Angles, CA; the host Washington DC and off course Wichita, KS
  • Stay Sharp for that 50 Years Uhuru Gala Dinner featuring Kilimanjaro Band-Wananjenje,Maestro King Kiki himself; Jahazi Modern Taarab and the talented Asia Idarius and her Tanzania Mitindo House.
To take advantage of early registration,  please visit www.dicotaus.org while there, we encourage you to access different links to familiarize yourself about DICOTA.

See you in Washington DC, this Sept 22nd-25th.

Ili uwe bora, tafuta kuwa bora kwanza! -2



WEWE ni sehemu ya All About Love, ukiacha kusoma hapa maana yake itakuwa haipo tena. Nimefurahi sana, maana umeendelea kuwa mdau wa ukurasa huu kila siku, safu ambayo kila kukicha inakuongezea kitu muhimu katika maisha yako ya kimapenzi.

Naam! Hata kama ulikuwa na ugomvi wa mara kwa mara na mwenzi wako, kolamu hii inakuongezea ujanja na unakuwa bora kwa mpenzi wako. Kama ni mara ya kwanza kuanza kusoma hapa, hutajuta na ninakukabirisha kwa moyo mkunjufu. Hii ni klabu ya wapendanao, ambao wana werevu wa masuala ya uhusiano na wanakubali kujifunza.

Ngoja nikuambie rafiki yangu, siri ya kuwa bora siku zote ni kujifunza. Karibu sana tujifunze pamoja. Mada ni kama inavyosomeka hapo, tulianza nayo wiki iliyopita, leo tunafikia tamati.

Nazungumzia juu ya mwenzi bora katika maisha ya mapenzi. Baadhi ya watu huwa wanalalamikia wenzi wao kuwa bora, lakini wanasahau jambo moja muhimu; ubora wa mwenzako ni matokeo ya wewe kuwa bora.

SALAAM ZA EID KUTOKA WASHINGTON METRO AREA

Wadau wa DMV wakiwa katika shamrashamra za Eid

Serikali kutolea tamko rasmi dawa ya Babu wa Loliondo




Serikali imeahidi kutoa tamko kuhusu taarifa za kitalaam zilizotolewa na Chama cha Madaktari nchini (MAT) kwamba dawa inayotolewa na Mchungaji mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapila, imeleta maafa kwa watumiaji.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda, aliyasema hayo jana alipotakiwa na NIPASHE kutoa taarifa ya serikali kuhusu kauli za MAT zilizotolewa hivi karibuni.
Katika taarifa yake, MAT ilisema wagonjwa wengi waliotumia dawa ya Babu inayotolewa kwenye kikombe, waliamua kuacha kutumia dawa zao za awali zilizotolewa hospitalini na hivyo kujikuta wakipata matatizo makubwa huku baadhi yao wakipoteza maisha.
Tangu tiba hiyo ianze kutolewa kwa maelfu ya Watanzania na wageni kutoka nje ya nchi, kumekuwepo na kauli za kupingana huku baadhi wakidai baada ya kuitumia walipona na wengine wakidai haikuwasaidia.

Igunga: Mkapa apata kombora la kwanza


Aambiwa ni mchafu asiyestahili kusimama jukwaani
  Kafumu naye apigwa kombora lake, ajibu mapigo
Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa
Wakati Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemteua Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, kwenda Igunga kuzindua kampeni za chama hicho za uchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo hilo unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2, mwaka huu, Chama Cha Wananchi (CUF) kimesema kiongozi huyo mstaafu amezingirwa na kashfa nyingi hivyo si mtu sahihi kusimama jukwaani katika kampeni hizo.
Akizungumza jana kutoka Igunga, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro, alisema Mkapa ni kati ya marais walionufaika na sekta ya madini, inayosimamiwa na mgombea wa CCM katika kinyang’anyiro hicho, Dk. Peter Kafumu, ambaye pia ni Kamishna wa Madini nchini.
Mtatiro alisema tambo za CCM katika kinyang’anyiro hicho, zinaonyesha namna ambavyo kisivyokuwa makini kwa kuwa Mkapa kama kada wa CCM, alijimilikisha kinyemela mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira kwa bei ya kutupa.

SALAAM ZA EID KUTOKA MICHIGAN

Saada na Anne

Balozi wa Libya afukuzwa Zimbabwe-BBC


Serikali ya Zimbabwe imemfukuza balozi wa Libya nchini humo ambaye wiki iliyopita alimuasi Kanali Muamamar Gaddafi na kuwaunga mkono waasi.
Rais Robert Mugabe
Taher Elmagrahi alijiunga na waandamanaji waliovamia ubalozi wa Libya mjini Harare na kupeperusha bendera ya waasi katika afisa za ubalozi mjini Harare.
Lakini Waziri wa mambo ya njee ya Zimbabwe amesema wao hawaitambui baraza la mpito la Libya .
Rais Robert Mugabe ni rafiki mkubwa wa Kanali Gaddafi ambaye alikuwa akiifadhili Umoja wa Afrika. Na ni mataifa machache ya Kiafriak ambayo yameitambua Baraza hilo la mpito la Libya.
Wiki iliyopita Serikali ya Zimbabwe ilipinga hatua ya Baraza la Umoja wa Mataifa la kuruhusu waasi wa Libya kupewa persa za serikali ya Libya.
Waziri wa Mambo ya Njee wa Zimbabwe Simbarashe Mumbengegwi ambaye ni wa chama cha Zanu-PF kinachoongozwa na Robert Mugabe amesema kuwa balozi huyo ana saa 72 pekee yake kuhama nchi.
"mara tu unapoasi mamalaka yaliokuchagua na kukua uwezo wa kuwa balozi na kuaanza kutii amri za watu wengine ... Inamaanisha kuwa tendo hilo linakupokonya haki ya kutambulika kama balozi", alisema
na juma lililopita alipotangaza kuunga mkono waasi bwana Elmagrahi alisema kuwe yeye sio balozi wa Gddafi ." nawakilisha watu wa Libya"
wanahabari wanasema kuwa Rais Mugabe na wapambe wake wanawasiwasi sana kufuatia mapindulizi yaliotokea nchini Libya.
Wanaharakati 40 walikamatwa mapema mwezi wa Februari baada ya kupatikana wakitazama video kuhusu mapinduzi ya Misri.
Bwana Mugabe ameishutumu NATO kwa kuingilia Libya akisema kuwa vita hivyo vilikuwa ni kwa sasabu ya mafuta.

LOOK OF THE DAY

Aida Issa From Washington,DC

Happy Birthday Omari B. Munisi . 6yrs

“Let the GOD decorate each golden ray of the sun reaching you with wishes of success, happiness and prosperity for you, wish you a Super Duper Happy Birthday Son.”

Rostam, Mkapa kuungana kampeni za CCM Igunga

ALIYEKUWA Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz ni miongoni mwa makada watakaotumiwa na CCM katika kampeni za kumsaka mrithi wake katika jimbo hilo.Habari zilizopatikana jana kutoka ndani ya kikao cha Kamati Kuu ya CCM (CC) kilichokutana juzi, Ikulu Dar es Salaam zinasema Rostam amepangwa kuhudhuria uzinduzi wa kampeni za CCM zitakaofanywa na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, Septemba 10, mwaka huu."Labda ratiba ibadilike, lakini ni kweli Rostam amepangwa kwamba ataambatana na Mzee Mkapa kwenda Igunga na yeye atabaki huko kama wiki moja hivi kusaidia kampeni hizo," alisema mmoja wa wajumbe wa Kamati Kuu hiyo ya CCM.

Tuesday, August 30, 2011

Stars yanoga Dar es Salaam


Image

WACHEZAJI wanaounda timu ya taifa ‘Taifa Stars’, wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi wamewasili kambini kwa ajili ya mchezo wa kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika dhidi ya Algeria utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Jumamosi ijayo.

Wachezaji waliowasili ni pamoja na Danny Mrwanda na Abdi Kassim wanaocheza soka la kulipwa nchini Vietnam katika klabu ya DT Long An, Mbwana Samatta anayekipiga TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kiungo Henry Joseph wa Konsivinger ya Norway, Athumani Machupa wa Vasuland IF ya Sweden na beki Idrissa Rajabu wa Sofapaka ya Kenya. 

Aua mwanawe aolewe-HABARI LEO

POLISI wilayani Bariadi mkoani hapa inamshikilia mwanamke mkazi wa kijiji cha Mwamabu wilayani humo kwa tuhuma za kumnyonga mtoto wake wa kumzaa ili aolewe.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Diwani Athumani, alisema ofisini kwake jana kuwa, Tabu Maimatha mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu ameuawa kikatili kwa kunyongwa na mama yake mzazi, akishirikiana na mpenzi wake, Kijiji Nyamagu ambaye alitoroka baada ya mauaji hayo.

Alimtaja mwanamke huyo kuwa ni Limi Limbu (22) mkazi wa kijiji cha Mwamabu kata ya
Bumera na kwamba tukio hilo lilitokea juzi saa saba za mchana kijijini hapo baada ya Limi kurubuniwa na mpenzi wake Nyamagu, kuwa wakimuua mtoto wake wataoana.

Baada ya kukamatwa, Limi alikiri mbele ya polisi kuwa alishirikiana na mpenzi wake huyo
kumwua mtoto wake, ili waishi kwa amani na waoane na kuanza maisha mapya katika ndoa yao.

Inadaiwa Limi baada ya kukubaliana na mpenzi wake huyo walifanya kitendo hicho cha kikatili ili kuondokana na bughudha ya mtoto huyo wa nje ya ndoa na hivyo wazae watoto wao wa ndani ya ndoa.

Kamanda Athumani alisema, katika tukio lingine lililotokea katika barabara ya Old Shinyanga saa 10 usiku wa kuamkia jana, mtu mmoja alikufa na wengine watatu kujeruhiwa vibaya baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugonga mti.

Alimtaja aliyekufa kuwa ni Jean Samson (44) mkazi wa Ngokolo mitumbani na majeruhi ni dereva wa gari hilo Emmanuel Kaleja (57), Mora Sendo ‘Choto’ (58) na Njile Chenya (43) wakazi wa Majengo mapya na Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga.

Alilitaja gari lililopata ajali kuwa ni Suzuki Escudo namba T 605 DHW na kuongeza kuwa majeruhi watatu wa ajali hiyo wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.

JK AKITOA SALAAM


Rais Jakaya Kikwete akitoa salamu kwa jumuiya ya Istqaama ya Tanzania, tawi la Dar es Salaam mara baada ya kushiriki katika futari iliyoandaliwa na jumuiya hiyo jijini Dar es Salaam. (Picha na Freddy Maro).

Majeshi ya Gaddafi yatakiwa kusalimu amri-BBC

Viongozi wa waasi wa Libya wamewapa majeshi yanayomwuunga mkono Kanali Gaddafi mpaka Jumamosi kusalimu amri au kukabiliana na majeshi.
Mustafa Abdul Jalil, anayeongoza Baraza la Mpito la Taifa (NTC), alisema onyo hilo limeelekezwa kwa wanaomtii Kanali Muammar Gaddafi waliopo mji alipozaliwa wa Sirte na katika miji mengine.
Tangazo hilo limetolewa baada ya mke wa Kanali Gaddafi na watoto wake watatu kukimbilia nchi jirani ya Algeria.
Algeria imejitetea kwa hatua hiyo waliochukua, huku waasi wakiita " kitendo cha kiburi".
Mpaka sasa mahala alipo Kanali Gaddafi haijulikani.
Wakati huo huo huo huko Libya, waasi wanajaribu kupambana na wanaomtii Gaddafi, na kujiandaa kusogea Sirte.

Natamani mfungo wa Ramadhani uendelee!

Wallah natamani mfungo uendelee. mume wangu kiranga kitupu haishi hodi hodi vijumbani. Ramadhani yote mume amekuwa mwadilifu na mwenye mapenzi bashasha, leo Ramadhani imekwisha moyo unanienda mbio, mume haishi vikao vya harusi na kulala matangani.  

Nimejitahidi kila kona kumdhibiti Bwana huyu bado sijafanikiwa; walimwengu nisaidieni  raha ya mume sina si kana kwamba simpendi mume wangu la hasha nampenda kwa mapana na marefu. Hodi hodi vijumbani zitakwisha lini? Mwezi mzima huu sikusikia nimechelewa kwenye kikao cha harusi wala nimelala kwenye matanga ya watani. 

Kila siku namuomba Mungu atunusuru sijui balaa hili litakwisha lini, ninauhakika safari ya Igunga kwenye kampeni za uchaguzi ipo njiani. Wapwani walisema mla mlaleo mlajana kala yani?
Nawatakia Eid njema,
 
Bilhuda Omar Abbas

NGUMI KUPIGWA UWANJA WA JAMUHURI MOROGORO IDI PILI

MABONDIA Asha Abubakar na Fadhila Adam wanatarajia kudundana katika pambano la kuhamasisha ngumi kwa wanawake litakalofanyika Idi pili katika Uwanja wa Jamuhuri, Morogoro.
Pambano hilo litakuwa ni miongoni mwa mapambano ya utangulizi katika pambano la marudiano kati ya mabondia wa ngumi za kulipwa Fransic Cheka na Mada Maugo.
Pambano hilo la ubingwa wa UBO linatarajia kuwa la raundi 10 uzito wa Middle huku likisimamiwa na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania,(PST).
Akizungumza Dar es Salaam jana, Promota wa ngumi hizo Kaike Siraju alisema, pambano hilo la kuhamasisha litakuwa la raundi 6 huku katika uzito wa Fly ambalo litakuwa ni moja ya pambano la kivutio siku hiyo.
"Wanawake ni wachache sana wanaoshiriki katika mchezo huu hivyo ni naimani watu watapata burudani ya kutosha kutoka kwa wadada hao," alisema kaike.
Alisema, kwa upande wa Maugo na Cheka kila bondia kajiandaa vya kutosha kwa ajili ya kuweza kuibuka na ubingwa ili aweze kuendeleza rekodi yake.

Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha  Rajabu Mhamila 'Super D', alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
"Ninatarajia kuwapelekea DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano la Cheka na Maugo ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi", alisema Super D.

SIKUKUU YA EID,WASHINGTON,DC,LEO AUG 30,2011

Msikiti wa Islamic Center uliopo Massachusetts Av,Washington,DC ndio uliswaliwa swala ya Eid Leo Aug 30.2011
Juu na chini ni Waumini wa dini ya Kislam waliojumuika pamoja msikitini hapo kuswali swala ya Eid
Waumini wa Dini ya Kislam wakibadilishana mawili matatu na huku wengine wakipeana mkono wa Eid
Ndugu zetu kutoka Somalia wakipeana mkono wa Eid
Nipongezi za Eid zikiendelea Msikitini hapo baada ya Swala ya Eid
Ndugu na marafiki waliokutana msikitini wakialikana kupata bwaba la Eid kama wanavyoonekana hapa 
Juu na chini ni pongezi za Eid zikiendelea.
Picha na Saleh Mohammed,Washington,DC
Kwa picha zaidi Bofya Read More

GQ HOLLYWOOD swagga,LABOR DAY WEEKEND,WASHINGTON,DC



Lobor Reunion/Eid El Fitr Weekend 3 dayz parties
Friday Sept 2,2011 KARIBU NITE @ TASTE LOUNGE,DC Free All Nite,
1812 Hamlin St,NE,
Washington,DC,20018

Sat Sept 3,2011 GQ HOLLYWOOD with LIVE PERFORMANCE @ TEATRO,
1909 K St,Nw,
Washington,DC
COVER $20

Sun Sept 4,2011 EAST AFRICAN SUMMER END NITE @ RIO LOUNGE,
13501 Baltimore Av,
Laurel,MD,20707
COVER $20
All Day,All Nite Free Nyama Choma

KARIBUNI,WASHINGTON,DC

Kitu usichokijua kuhusu ‘juisi ya boksi’

BILA shaka unapoingia dukani au supermarket kununua juisi ya box, huwa unaamini kuwa iliyoandikwa ‘100% Puer Juice’ huwa ni halisi na ndiyo bora. Kwa kukuongezea imani zaidi, watengenezaji wameweka na neno ‘No Sugar Added’  au ‘No preservatives’ (haikuongezwa sukari wala dawa)!

Kuanzia leo elewa kwamba hayo ni maneno ya kibiashara tu, ukweli hauko hivyo! Umewahi kujiuliza kwa nini maboksi yote ya juisi hiyo yawe na ladha moja tu. Sote tunajua kwamba, kama ni juisi ya machungwa kwa mfano, ukila machungwa matano, yote hayawezi kuwa na ladha moja!

REMINDER: 2 Days left .....2011 DICOTA....

YOU have only 2 days left to take advantage of $99.00 early registration fee for this year's DICOTA Convention!!!!! It will be $190 from Sept 1st to Sept 20th when doors will be closed.

Few Highlights for this Year's Convention includes (but not limited to):
  • Investments Opportunities and Role of the Diaspora: Learn what role does National Social Security Fund (NSSF), Tanzania Investment Center (TIC), Z'Bar Investment Promotion Agency (ZIPA), Tanzania Revenue Authority (TRA) plays to facilitate engagement and participation in development in Tanzania. Learn how you can utilize Diaspora Desk in our Foreign Affairs & International Cooperation Office.
  • Have a clear understanding on the Role of Central Bank (BOT) and other Commercial Banks in facilitating effective Diaspora Remittances and Providing Capital for Investments. Key figures from BOT, Stanbic Bank Tanzania, CRDB Bank and National Housing Corporation (NHC) to name a few will engage in panel discussion and presentations.
  • USA vs Tanzania Bilateral relations: Familiarize yourself with Millennium Challenge Corporation (MCC) grant and what it has achieved in building Tanzania's infrastructure. 
  • Loan Financing Small and Medium Scale Economic Projects Opportunities for Diaspora?: International Finance Corporation (IFC) World Bank Group will be sending their Country Lead on the subject.
  • Diaspora Access to Land?: The Who Is Who panelist: Mr. Kyando Mchechu-NHC Director General, Dr. Ramadhani Dau-NSSF Director General, Nyumba Poa Ltd Director Mr Peter Malika, to name a few will quest our thirst on the subject. Permanent Secretary Ministry of Land and Housing Development (Ardhi) will present Government plans to assist Diaspora in accessing land in Tanzania.
  • Ever wonder about Employment Opportunities and Challenges for Diaspora Skills Engagement? Radar Recruit CEO will do a presentation on this...and Yes please, BRING YOUR RESUMES!!
  • Do YOU: DICOTA has set aside half a day on Sept 25th for Networking and Job Interviews !
  • Long weekend? How about Maasai BBQ @ the Park, Soccer Bonanza featuring sharp skills from H-Town, TX; Twin Cities, MN; Seattle, WA; City of Angles, CA; the host Washington DC and off course Wichita, KS
  • Stay Sharp for that 50 Years Uhuru Gala Dinner featuring Kilimanjaro Band-Wananjenje,Maestro King Kiki himself; Jahazi Modern Taarab and the talented Asia Idarius and her Tanzania Mitindo House.
To take advantage of early registration,  please visit www.dicotaus.org while there, we encourage you to access different links to familiarize yourself about DICOTA.

See you in Washington DC, this Sept 22nd-25th.

Bado unaamini mwanamke akitongoza ni malaya?

NI dunia na mambo ya kisasa. Chapuo la mabadiliko linazidi kupata meno makali. Zamani ilionekana mwanamke akitongoza ni haramu lakini sasa mambo ni bambamu. Mtu yake kauli, moyo ukivutika, haraka sana anatua mzigo kwa mhusika.

Vipi ubaki na jakamoyo wakati anayekufanya moyo wako ufukute yupo karibu? Hii ni mada ambayo nilianza nayo wiki iliyopita, mastaa wakubwa Bongo, Stara Thomas, Sakina Lyoka, Tayana Tibenda, Sauda Mwilima na Latifa Idabu ‘Badra’ walieleza mitazamo yao.

Rage, Saad Kawemba wazikunja TFF


TFF yaigomea Yanga nembo mpya Voda
Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage
Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, alikaribia kuzipiga na Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Saad Kawemba, nje ya ofisi za TFF jana baada ya kutokea kutoelewana kwa wawili hao.
Taarifa kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo zilidai kuwa kutofautiana kwa wawili hao kulifuatia maneno ya dharau yaliyotolewa Rage kuhusu suala la uhamisho wa mshambuliaji wa Simba, Gervais Kago, ambaye tishio la kuzuiwa kwake kucheza mechi ya Ngao ya Hisani dhidi ya Yanga, lilihatarisha kutofanyika kwa mechi hiyo ambayo Wekundu wa Msimbazi walikuja kushinda 2-0.
Rage, ambaye aliitwa TFF pamoja na Afisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu, ili wakajieleze kwa kauli zao za kutishia kugomea mechi hiyo, alidaiwa kutoa kauli hiyo ya dharau akiwa mbali na Kawemba lakini kiongozi huyo wa TFF alifikishiwa taarifa hizo na akatoka ndani ya ofisi aliyokuwa wa shirikisho hilo na kuja moja kwa moja kutaka kumvaa Rage na ndipo kizaazaa kilipozuka na watu kuanza kujaa kabla ya Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah na Sendeu kuwaamua wawili hao.

THE TEN MINUTES FIX EP 6

Familia ya Gaddafi yatorokea Algeria-BBC

Mke na watoto watatu wa kiongozi wa Libya aliye mafichoni Muammar Gaddafi wako nchini Algeria, maafisa wa Algerian wamesema.
Taarifa ya wizara ya mambo ya nje imesema mke wa kanali Gaddafi, Safia, binti yake Ayesha na watoto wa kiume Muhammad na Hannibal waliondoka Libya mapema Jumatatu.

Sita wafa, wabaki majivu baada gari kuteketea moto

Joyce Joliga
WATU sita wameteketea kwa moto na kubaki majivu baada ya gari walilokuwa wamepanda aina ya Land Rover kuacha njia na kuingia kwenye korongo kisha kuwaka moto.Tukio hilo lilitokea juzi saa 12:00 jioni katika Kijiji cha Chunya karibu na mji mdogo wa Mbamba Bay, wilayani Mbinga na watu hao hawajafahamika hata jinsi zao.

Kamanda wa Polisi wa Ruvuma, Michael Kamuhanda alisema gari aina ya Land Rover 110 lilikuwa likiendeshwa na dereva, Stephen Ngoko (32).

Kamanda Kamuhanda alisema gari hilo lilikuwa likitokea Mbinga kwenda Mbamba Bay na kwamba abiria wawili walijeruhiwa na wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mbuyula.

Aliwataja majeruhi hao kuwa ni Jeremia Masalo (39), Mtanzania anayeishi Msumbiji pamoja na mtoto Anna Geofrey (3), mkazi wa Mbinga.

CAG: Sina hofu ya uchunguzi wa Bunge kwa Jairo


Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh
Ramadhan Semtawa
MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh amesema hana hofu juu ya uchunguzi unaotarajiwa kufanywa na Kamati ya Bunge kuhusiana na tuhuma za Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo.

Kauli hiyo ya kwanza ya Utouh imekuja wakati Kamati hiyo teule iliyotangazwa na Spika, Anne Makinda Ijumaa iliyopita inatarajiwa kuanza kukutana Jumatatu ijayo.

Huku uchunguzi huo mpya wa Bunge unaotarajiwa kuchukua wiki nane ukiibua mjadala mzito nchini kwa watu wa kada tofauti wakiwamo wasomi, CAG Utouh alisema hana shaka nao kwani kila upande unafanya uchunguzi kwa kutumia hadidu zake za rejea.

CCM, Chadema anga kwa anga Igunga


*CC YA  CCM WAMPITISHA  ALIYEKUWA MPINZANI WA ROSTAM, MKAPA KUZINDUA KAMPENI
Leone Bahati
KAMATI Kuu (CC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imemtangaza Dk Dalaly Kafumu kuwa mgombea wake katika uchaguzi mdogo wa Igunga huku pia kikitangaza kutumia helikopta kupiga kampeni za anga kwa anga ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha jimbo hilo haliangukii kwenye himaya ya upinzani.

Hatua ya CCM kutangaza kutumia helikopta inakuja wakati tayari Chadema, nacho tayari kikiwa kimetangaza kutumia usafiri huo wa anga kufika maeneo mengi katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2 kuziba nafasi ya Rostam Aziz, aliyejiuzulu wadhifa huo mnamo mwezi Julai.

SALAAM ZA IDD

EID MUBARAK from Mustafa Hassanali & Team


Notting Hill Carnival 2011



URBAN PULSE inawaletea video fupi ya Notting Hill carnival iliyofanyika jumapili 28.8.11
Asanteni,

URBAN PULSE CREATIVE wakishiriana Miss Jestina Blog

AUAWA KIKATILI NA WANANCHI WENYE HASIRA KALI KWA KUIBA KUKU

Marehemu NASIB EXZAVERY maalufu kama Mkemia akiwa amechomwa moto eneo la viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge Jijini Mbeya kwa kosa la wizi wa kuku ambaye Mwenye Kuku huyo hajafahamika
Marehemu NASIB pamoja na Kuku waliodaiwa kuwaiba na kumsababishia kifo.
Jeshi la Polisi likiwa limefika eneo la Tukio kuuchukua Mwili wa marehemu na kuupeleka katika hospitali ya Rufaa mkoani Mbeya
Gari hili ndilo linalodaiwa kuwa marehemu alikuwa akifanya kazi kama Utingo
Watoto wa shule ya Msingi Mwenge wakiwa eneo la Tukio.

Picha kwa hisani ya Mbeya yetu Blog

Ibada ya Kiswahili Columbus OH Septemba 4