ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 31, 2010

Arsenal wapigana kufa kupona dhidi ya Barca


  Lionel Messi (R) of Barcelona is pursued by Cesc Fabregas of Arsenal during the UEFA Champions League quarter final first leg match between Arsenal and FC Barcelona at the Emirates Stadium on March 31, 2010 in London, England.    
Andrey Arshavin #23 of Arsenal is substituted early in the first half by team mate Emmanuel Eboue during the UEFA Champions League quarter final first leg match between Arsenal and FC Barcelona at the Emirates Stadium on March 31, 2010 in London, England.
Wesley Sneijder of FC Internazionale Milano is challenged by Aldonin Evgeny of CSKA Moscow during the UEFA Champions League Quarter Finals, First Leg match between FC Internazionale Milano and CSKA Moscow at Giuseppe Meazza Stadium on March 31, 2010 in Milan, Italy.
Maicon (L) of FC Internazionale Milano is challenged by Mamaev Pavel of CSKA Moscow during the UEFA Champions League Quarter Finals, First Leg match between FC Internazionale Milano and CSKA Moscow at Giuseppe Meazza Stadium on March 31, 2010 in Milan, Italy.
Baada ya kulemewa kwa maarifa na Barcelona mnamo  cha kwanza, Arsenal walipambana kufa na kupona kutoka sare 2-2 katika uwanja wao wa Emirates.
Arsenal wangali na kibarua kigumu watakaposafiri hadi Uhispania kwa mechi ya marudio mnamo wiki mbili zijazo.
Katika mechi nyingine ya robo fainali Inter Milan iliitandika CSKA Moscow 1-0.
Barcelona walifanya mashambulizi makali mnamo kipindi cha kwanza huku Arsenal wakibaki kumshukuru kipa Manuel Almunia kwa kuwaokoa.
Hata hivyo uhodari wa Almunia ulitiwa dosari pindi tu kipindi cha pili kilipoanza.
Alifanya kosa la kuondoka kwenye goli na kumwachia mshambulizi Zlatan Ibrahimovic kumimina bao la kwanza.
Ibrahimovic aliongeza la pili huku matumaini ya Arsenal kudhibiti mchezo yakididimia.
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger alimwondoa Bacary Sagna na kumwachilia Theo Walcott kuwatatiza walinzi wa Barca.
Baada ya muda mfupi Walcott aliipatia Arsenal bao la kwanza.
Nahodha Cesc Fabregas aliongeza bao la pili kupitia penalti baada ya kuchezewa vibaya na Carles Puyol ambaye alitimuliwa kwa kadi nyekundu.

Aliyechoma makaburi Uganda ajisalimisha


Mtu mmoja amejisalimisha kwa polisi nchini Uganda na kukiri kuchoma moto makaburi ya wafalme wa kimila wa Baganda mapema mwezi huu.
Mtu huyo anadai aliambiwa achome makaburi kwa njia ya maono na kusema makaburi yalikuwa ya kishetani.
Falme hiyo ya Baganda ina ushawishi mkubwa na moto huo uliibua ghasia ambapo majeshi ya usalama yalifyatua risasi na kuua watu watatu.
Polisi wamesema wanachunguza afya yake ya kiakili.
Buganda ni falme kubwa kati ya nne zilizopo Uganda, zote ambazo hazina nguvu ya kisiasa.
Mabishano juu ya eneo baina ya Mfalme wa Baganda Ronald Mutebi na
Rais Yoweri Museveni kulisababisha ghasia mwaka 2009.

Waasi wa Chechnya wadai kulipua Moscow


  
Kiongozi wa kundi la waasi wa Chechnya, Doku Umarov, amesema kundi lake lilihusika la mashambulio mawili ya mabomu kwenye treni za chini ya ardhi mjini Moscow, ambako watu 39 waliuawa.
Katika ujumbe wa video uliowekwa kwenye tovuti ya waasi wa Chechnya, alisema yeye binafsi aliagiza kufanyika mashambulio hayo.
Alisema mashambulio yalifanyika kulipiza kisasi dhidi ya majeshi ya Urusi mwezi Februari, yaliyoua "Wachechen wasio na hatia" na ameionya Urusi ijiandae kwa mashambulio zaidi.
Wachunguzi wa Urusi wamesema wanaamini walipua mabomu wawili wa kujitolea muhanga ambao ni wanawake walihusika na wanahusiana na wanamgambo wa eneo la North Caucasus.
Waziri Mkuu Vladimir Putin ametoa wito kwa majeshi ya usalama "kuwaangamiza" wale waliohusika na mashambulio.

ICC yaamua ghasia za Kenya zichunguzwe

Ghasia zilizuka baada ya uchaguzi
Ni rasmi kwamba wahusika wakuu wa machafuko yaliyozuka nchini Kenya baada ya uchaguzi mkuu wa 2007 watachunguzwa na kufunguliwa mashtaka.
Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ilimpa idhini mwendesha mashtaka mkuu Luis Moreno-Ocampo kufanya uchunguzi na kuwafungulia mashtaka washukiwa wakuu 20.
Ghasia zilizuka baada ya vyama vikuu nchini humo, PNU na ODM, kutofautiana kuhusu matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.
Watu zaidi ya 1,300 waliuawa na wengine zaidi wakapoteza makazi yao.
Majaji wawili kati ya watatu waliamua kwamba huenda uhalifu dhidi ya binadamu ulitendwa.
"Taarifa zilizopo zinatosha kudhihirisha kwamba uhalifu dhidi ya binadamu ulitendwa nchini Kenya," waliamua majaji hao.
Lakini jaji mmoja alitofautiana na wenzake kuhusu uamuzi huo.
Akiwasilisha ombi lake kwa majaji mwezi Novemba mwaka jana, Luis Moreno Ocampo alidai kwamba viongozi wa kisiasa walipanga na kufadhili machafuko hayo.
Wakenya wengi wamepongeza uamuzi huo wakisema ni njia moja ya kumaliza mtindo wa kutenda uovu bila kujali.

Mahakama ya kiislamu Nigeria yakataza Twitter


Twitter
 Mahakama moja ya kiislamu nchini Nigeria imeipiga marufuku kundi moja la kutetea haki za binadamu kwa kuwa na mjadala kwenye wavuti juu ya kutoa adhabu ya kukatwa viungo.
Hatua hii inafuatia agizo la muda lililotolewa wiki iliyopita na mahakama kaskazini mwa Nigeria kuzuia mtandao wa Facebook na Twitter kutumiwa kujadili suala hilo.
Awali marufuku hiyo ilipendekezwa na kundi moja linalounga mkono Sharia lililosema wavuti zitatumika kukejeli sheria za kiislamu.
Sheria za kiislamu zinafuatwa pamoja na sheria zisiokuwa na uhusiano wa kidini katika majimbo 12 kati ya 36 nchini humo.

Wapinzani Sudan kuamua kuhusu uchaguzi


 
Viongozi wa makundi ya upinzani nchini Sudan wanakutana kujadili ikiwa watashiriki katika uchaguzi uliopangwa kufanyika tarehe 16 April.
Tayari wajumbe wa chama cha SPLM wanakutana kujadili msimamo wao kuhusu uchaguzi huo.
Makundi ya upinzani ya kaskazini mwa nchi hiyo tayari yametoa wito uchaguzi huo uhairishwe kutokana na hofu kwamba hautakuwa wa hura na haki.
Mazungumzo ya leo huenda yakasababisha kundi la waasi wa zamani wa kusini mwa sudan, SPLM, kuungana na makundi hayo kususia uchaguzi.
Uchaguzi wa April utakuwa ni uchaguzi wa kwanza kuwahi kufanyika nchini sudan kwa kipindi cha miaka 24 iliyopita.

12 wauwawa kwa mabomu Urusi

Wachunguzi wakusanyika katika eneo  la mkasa
Mabomu mawili yaliyolipuliwa na mlipuaji wa kujitolea mhanga katika eneo la Urusi la Dagestan - Kaskazini mwa Caucasus, yamewaua watu 12, miongoni mwao akiwa kiongozi wa jeshi la polisi na maafisa wake kadhaa.
Mmoja wa walipuaji hao alitegua bomu lake aliposimamishwa na maafisa wa polisi na kuamrishwa kuliegeza gari lake pembeni.
Mwingine aliyekuwa amevalia sare rasmi za polisi, alijilipua alipokuwa akikaribia mahali ulipotokea mlipuko wa kwanza.
Waziri Mkuu wa Urusi, Vladmir Putin, amesema kuwa milipuko hiyo huenda ina uhusiano na milipuko mingine miwili iliyowaua watu 39 mjini Moscow Jumatatu.
                   MSIBA




Familia ya Mzee Augostino Lissu Mughwai wa Mahambe, Singida inasikitika kutangaza kifo cha mama  yao mpendwa Martha Alu Alute kilichotokea tarehe 30 Machi, 2010 huko Dar es Salaam, Tanzania. Maandalizi yanafanywa kusafirisha mwili wa marehemu Mahambe, Singida kwa mazishi. 

Marehemu alizaliwa mwaka 1932 Ighuka, Singida. Ameacha mume na watoto nane: Alute Mughwai wa Arusha, Tundu Lissu, Mjengi Lissu na Christina Lissu wa Dar es Salaam, Rose Masesa wa Songea, Peter Muro Mughwai wa Kondoa, Mateo Mughwai wa Singida na Vincent Lissu Mughwai wa Connecticut, Marekani. 

Vile vile marehemu ameacha wajukuu 20, na vitukuu 6.

Kwa marafiki wa wafiwa wanaokaa nje ya Tanzania (Marekani, Uingereza n.k) unaweza kutuma rambirambi zako kwenye accnt # 1259458568, routing #221172610.

Au kwenye anwani ifuatayo: Vincent Mughwai 370 Huntington Road 2F Bridgeport CT 06608

Afisa ubalozi, mgeni rasmi Simba na Yanga,Dc


                      Simba (Lunyasi)


Afisa ubalozi amekubali mualiko kuwa mgeni rasmi kwenye kindumbwe dumbwe cha Simba na Yanga,mechi inayozungumziwa mjini Washinngton na vitongoji vyake,
                                           Yanga Imara



Mpambano huo wa kukata na shoka utachezwa jumapili April 4 kwenye wanja jipya la 1417 Kalmia St,Nw,Washington Dc,kambi zote zipo shwari na zinaendelea vizuri na mazoezi.Simba inaonekana imejiimarisha zaidi baada ya wachezaji wengi wa mikoani akiwemo Francis Makalaa aliyewahi kuichezea Simba miaka ya Nyuma kuthibitisha kuwepo kwenye mpambano huo,Kuhusu Nteze John bado viongozi wa Simba wanaendelea kumtafuta kwa udi na uvumba,Nteze anaishi Washington State alisahawahi  kua mchezaji wa kutumainiwa Simba na Timu ya Taifa.kabla hajajiunga na Simba,alikua mchezaji wa Pamba ya Mwanza.

                             Stars United

Kambi ya Yanga imekua kimya Kocha Yasini Randi amesema Simba wacha waongee,msema ukweli dakika 90,sisi bwana tupo tunaendelea vizuri na kambi yetu,sisi tunaingia uwanjani kama YANGA IMARA KUFUNGWA DAIMA MWIKO

Jumamosi April 3 kutakua na mechi nyingine ya Stars na Maryland untd,itakayochezewa 

18031 central park circle,
 Boyds,Md,20841,uwanja # 20

mechi hii ni moja ya mechi za kujinoa ya Stars kwa safari ya kuelekea Sweden july mwaka huu,mechi nyingine ya Stars ni April 24 mjini Boston itapambana na Zambia
                    Maryland United

Tuesday, March 30, 2010


Maximo na kijasho chembamba


Mara baada ya kuicharaza timu ya Somalia mabao 6-0, Kocha Mkuu wa timu ya taifa 'Taifa Stars' Marcio Maximo azidi kuwahofua wapinzani wake Rwanda, Amavubi watakayokutana nao uso kwa uso hapo Mei Mosi hapa kwa Lukuvi.



Maximo alisema kwamba ile safari ya kuelekea katika fainali zijazo cha Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN, inatarajiwa kuanza pindi watakapokutana na Rwanda na kwamba mechi hiyo ya juzi ilikuwa ni kama mazoezi.

Alisema kwa sasa timu yake ina kazi kubwa ya kuhakikisha wanaifunga Rwanda, ili kuweza kupata tiketi hiyo ya kushiriki katika fainali hizo za pili zitakazofanyika nchini Sudan mwakani.

"Rwanda wana timu nzuri na mara nyingi huwa na ushindani tunapokutana. Fainali yetu itakuwa ni Kigali tutakaporudiana na si katika mechi ya kwanza itakayofanyika hapa nchini. Nadhani kila shabiki anaifahamu Rwanda inapokuwa nyumbani kwao," alisema Maximo.

Timu ya Stars itazidisha mazoezi katika kujiandaa na mechi hizo mbili, na wanaamini kwamba kila mchezaji anafahamu ugumu unaokuwepo wanapokutana na Rwanda.

Alisema kwamba wakati wote walipokuwa wanajiandaa na Somalia, mawazo ya wote yalikuwa yako mbele zaidi kwa kuitazama Rwanda, kwa sababu walifahamu kwamba ndipo mahala ambapo mashindano hayo yanaanza rasmi kwao.

Kwani mechi ya Stars na Rwanda itakuwa ngumu kutokana na timu hizi kufahamiana zaidi, huku kila timu ikipata ushirikiano mkubwa kutoka katika serikali yake.

Naye Nahodha wa Stars, Nadir Haroub 'Cannavaro', alisema kwamba wao wana uzoefu na mechi za kimataifa tofauti na wachezaji wa Rwanda ambao wengi wametoka katika timu ya vijana ya U-20 ya nchi hiyo.

Cannavaro alisema kwamba mwaka huu wako makini zaidi na hasa ukizingatia kwamba fainali hizo husaidia kuwatangaza wachezaji.

Stars na Rwanda iliyokuwa chini ya mzawa, Eric Nshimiyimana, mara ya mwisho zilikutana katika hatua ya nusu fainali ya Kombe la Chalenji yaliyofanyika Desemba mwaka jana jijini Nairobi Kenya, ambapo Kilimanjaro Stars ilikubali kipigo cha magoli 2-0.

Na timu mbili za ukanda huu ambapo ni mshindi baina ya Taifa Stars na Amavubi, na wa mechi nyingine baina ya The Cranes na Harambee Stars ya Kenya, ndio zitawakilisha ukanda wao katika fainali zijazo za CHAN.




Uwanja wa ndege wafungwa,Kisa PANYABUKU!

Mkuu wa wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, Queen Mlozi ameiomba serikali ya JK kuitengea wilaya hiyo fedha angalau kiduchu ktk bajeti ya mwaka huu ili waweze kukarabati uwanja wao wa ndege ambao umeathiriwa ile mbaya na panyabuku kiasi cha kuamuliwa ufungwe.

Uwanja wa Ndege wa Nkilizya ulifungwa mwaka 2007 baada ya ndege ndogo tatu kuharibika wakati zikitua uwanjani hapo kutokana na njia ya uwanja huo kujaa mashimo ambayo ni makazi ya kudumu ya panyabuku hayo.

Ombi hilo limetolewa na mkuu huyo wa wilaya wakati alipokuwa akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawlance Masha alipotembelea na kukagua eneo la uwanja huo kujionea hali ya usafiri wilayani Ukerewe

Madawati yamchanganya Mkuu wa Mkoa

SPW: Ikuna village primary school, Tanzania 
WANAFUNZI 485 kati ya wanafunzi 685 wa Shule ya Msingi Ilala iliyopo mita 400 kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa wanasoma wakiwa wamekaa chini kutokana na uhaba wa madawati shuleni hapo.

Kwa zaidi ya miaka minne jitihada za shule hiyo kuwashirikisha wazazi wa wanafunzi kutatua kero hiyo zimekuwa zikigonga mwamba.

Akiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Getrude Mpaka, Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Aseri Msangi na viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wakiwemo wa Idara ya Elimu, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mohamed Abdulaziz jana alifanya ziara ya ghafla shuleni hapo kujionea hali halisi.

Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkuu wa Shule hiyo, Agustino Chazua ilibainisha kwamba shule hiyo ina madawati 100 tu ambayo kiutaratibu yanatosheleza wanafunzi 200 tu, ilimsikitisha Mkuu huyo wa Mkoa.

Kwa masikitiko makubwa, Mkuu wa Mkoa wa Iringa aliyeonekana kukerwa na uchakavu wa vyumba vya madarasa ya shule hiyo na idadi kubwa ya wanafunzi wanaokaa chini wakati wakifundishwa, aliahidi kuchangia Sh milioni moja kwa ajili ya ununuzi wa madawati na mifuko hamsini ya saruji kutoka katika ofisi yake huku Mkuu wa Wilaya naye akichangia.

Katika moja ya vyumba vya madarasa vya shule hiyo, HabariLeo ilishuhudia wanafunzi watano wakiwa wameminyana kwenye dawati lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi wawili.

Chazua alisema mahitaji halisi ya madawati shuleni hapo ni 350 na hivyo kufanya upungufu uwe madawati 250.

Mkuu wa Wilaya Iringa hata hivyo alisema wamekubaliana na wazazi wote wa shule hiyo kuchangia Sh 12,600 kila mmoja ili kukabili tatizo hilo kutokana na kikao chao cha Machi 27 mwaka huu

Waganga wa jadi wapigwa ‘wakifufua’ watoto

WAGANGA wawili wa jadi waliotaka kufufua watoto wawili waliokufa maji bwawani, wamepigwa na wananchi na kulazwa kwenye kituo cha afya cha Mtimbila wilayani Ulanga, mkoani hapa.


Waganga hao, Wanda Mazayani (62) na Masunga Kapunga (43), walikumbana na kipigo hicho juzi, baada ya kuchukua fedha kutoka kwa mzazi wa watoto hao na kuanza uganga ili kuwafufua mbele ya wananchi hao.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Thobias Andengenye, alisema jana kuwa wananchi hao walikerwa na udanganyifu wa waganga hao kwamba wanaweza kuwafufua huku wakimtaja mtu kwamba amewaua kwa imani za kishirikina, wakati ukweli ni kuwa walikufa maji.

Akielezea kwa undani juu ya tukio hilo, Kamanda alisema juzi saa 7 mchana katika eneo la Likea, wanafunzi hao wa familia moja wa shule ya msingi Isangule, Leticia John (12) ambaye ni wa darasa la nne na mdogo wake Flora (8) wa darasa la pili, walipoteza maisha baada ya kutumbukia bwawani humo.


Kamanda Andengenye alisema mauti hayo yaliwakuta watoto hao wakati wakipita katikati ya mabwawa mawili ya maji kwenye eneo hilo, ndipo mtoto mmoja alipoteleza na kutumbukia kwenye bwawa mojawapo.

Baada ya mtoto huyo wa darasa la pili kutumbukia bwawani, dada yake alijaribu kumwokoa kwa kumvuta mkono na bahati mbaya naye akatumbukia na kuzidiwa maji na kufikwa na mauti hayo.

Kilichofuata ni baba mzazi wa watoto hao, John Kikula, kuhusisha tukio hilo na imani za kishirikina. Kutokana na imani hiyo, mzazi huyo alikwenda kwa waganga hao ambao walimweleza kuwa chanzo cha vifo vya watoto hao, ni mkazi wa tarafa hiyo (jina linahifadhiwa).

Mbali na kumweleza hayo, pia waganga hao walihitaji fedha kwa ajili ya kuwafufua watoto hao, wakalipwa kiasi ambacho hakikujulikana mara moja na kisha kufuatana na mzazi huyo, na baadhi ya ndugu hadi eneo la tukio.

Wakiwa eneo hilo, waganga wakianza uganga ili kuwafufua watoto hao, ndipo baadhi ya wananchi walipofika kushuhudia tukio hilo na kuingiwa na hofu na kuwashambulia waganga hao.

Polisi walifika eneo hilo na kuwaokoa waganga hao na kuwapeleka kulazwa kwenye kituo cha afya Mtimbila. Polisi inashikilia wazazi wa marehemu hao na wananchi walioshiriki mashambulizi dhidi ya waganga hao.

Lyon 3-1 Bordeaux - UEFA Champions League

Marouane Chamakh (r) of Bordeaux misses a chance with a header as Lyon goalkeeper Hugo lloris is stranded during the Lyon v Bordeaux UEFA Champions League quarter-final 1st leg match at the Stade Gerland on March 30, 2010 in Lyon, France.
Marouane Chamakh (r) of Bordeaux misses a chance with a header as Lyon goalkeeper Hugo lloris is stranded during the Lyon v Bordeaux UEFA Champions League quarter-final 1st leg match at the Stade Gerland on March 30, 2010 in Lyon, France
Marouane Chamakh (r) of Bordeaux scores his sides first goal during the Lyon v Bordeaux UEFA Champions League quarter-final 1st leg match at the Stade Gerland on March 30, 2010 in Lyon, France.
Marouane Chamakh (r) of Bordeaux scores his sides first goal during the Lyon v Bordeaux UEFA Champions League quarter-final 1st leg match at the Stade Gerland on March 30, 2010 in Lyon, France.
Yoan Gouffran (c) of Bordeaux is sandwiched between Aly Cissokho (l) and Mathieu Bodmer (r) of Lyon during the Lyon v Bordeaux UEFA Champions League quarter-final 1st leg match at the Stade de Gerland on March 30, 2010 in Lyon, France.
Yoan Gouffran (c) of Bordeaux is sandwiched between Aly Cissokho (l) and Mathieu Bodmer (r) of Lyon during the Lyon v Bordeaux UEFA Champions League quarter-final 1st leg match at the Stade de Gerland on March 30, 2010 in Lyon, France

Arsenal & Barcelona Training Session

Lionel Messi of Barcelona during a training session ahead of their UEFA Champions League quarter final first leg match against Arsenal at the Emirates Stadium on March 30, 2010 in London, England.Gerard Pique of Barcelona during a training session ahead of their UEFA Champions League quarter final first leg match against Arsenal at the Emirates Stadium on March 30, 2010 in London, England.Thierry Henry of Barcelona during a training session ahead of their UEFA Champions League quarter final first leg match against Arsenal at the Emirates Stadium on March 30, 2010 in London, England.Josep Guardiola the Barcelona coach during a training session ahead of their UEFA Champions League quarter final first leg match against Arsenal at the Emirates Stadium on March 30, 2010 in London, England.(L-R) Carlos Vela, Thomas Vermaelen, Tomas Rosicky, Emmanuel Eboue and Denilson of Arsenal warm-up during Arsenal training ahead of their UEFA Champions League quarter final first leg match against Barcelona at London Colney on March 30, 2010 in St Albans, England.(L-R) Thomas Vermaelen, Tomas Rosicky and Eduardo of Arsenal warm up during Arsenal training ahead of their UEFA Champions League quarter final first leg match against Barcelona at London Colney on March 30, 2010 in St Albans, England.Arsene Wenger the Arsenal coach watches his players train during an Arsenal training session at London Colney on November 23, 2009 in St Albans, England.

Bayern Muenchen 2-1 Manchester United - UEFA Champions League


Ivica Olic of Bayern Muenchen challenges Darren Fletcher of Manchester United during the UEFA Champions League quarter final first leg match match between Bayern Muenchen and Manchester United at the Allianz Arena on March 30, 2010 in Munich, Germany.
Ivica Olic of Bayern Muenchen challenges Darren Fletcher of 
Manchester United during the UEFA Champions League quarter
 final first leg match match between Bayern Muenchen and 
Manchester United at the Allianz Arena on March 30, 2010 in Munich, 
Germany
Franck Ribery of Bayern Muenchen challenges Gary Neville of Manchester United during the UEFA Champions League quarter final first leg match match between Bayern Muenchen and Manchester United at the Allianz Arena on March 30, 2010 in Munich, Germany.
Franck Ribery of Bayern Muenchen challenges Gary Neville of 
Manchester United during the UEFA Champions League quarter final 
first leg match match between Bayern Muenchen and 
Manchester United at the Allianz Arena on March 30, 2010 in Munich,
 Germany.
A sign displaying "Hate Glazer" in among the Bayern fans during the UEFA Champions League quarter final first leg match between Bayern Muenchen and Manchester United at the Allianz Arena on March 30, 2010 in Munich, Germany.
A sign displaying "Hate Glazer" in among the Bayern fans during 
the UEFA Champions League quarter final first leg match between
 Bayern Muenchen and Manchester United at the Allianz Arena on
 March 30, 2010 in Munich, Germany

Mbunge wa CCM ahamia upinzani


Image
Mbunge wa Kishapu kwa tiketi ya CCM, Fred Mpendazoe, (Katikati) akiwa katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jana wakati akitangaza kujiunga na Chama Cha Jamii (CCJ), Picha na Mwandishi Wetu
Katika tukio nadra, chama tawala nchini Tanzania, CCM, kimepoteza mbunge mmoja ambaye amehamia chama kipya cha upinzani.
Mbunge huyo, Fred Mpendezoe, ametangaza kujiunga na Chama Cha Jamii yaani CCJ kilichopewa usajili wa muda hivi karibuni.


Bw Mpendazoe amekuwa miongoni mwa wabunge wenye kukosoa wazi hitilafu ndani ya CCM. Kumekuwa na uvumi mwingi kwamba chama hicho kitazoa vinara wa CCM.
Hata hivyo, chama chake alichokihama, kimesema hakiona lolote la ajabu kutokana na hatua ya Bw Mpendazoe.
Makamu wa mwenyekiti wa CCM, Bw Pius Msekwa, alipohojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya BBC, alisema kuondoka kwa Bw Mpendazoe ni kama mto Rufiji kupoteza ndoo moja tu ya maji, na kamwe hilo ni jambo ambalo halitakiathiri chama kwa njia yoyote.
Vile vile alisema mbunge huyo ana uhuru wa kukihama chama, kulingana na katiba ya CCM.

Urusi yaomboleza rasmi


Warusi wanaomboleza
Watu 39 waliuawa katika mashambulio mawili ya Jumatatu

Huku Urusi ikiwakumbuka rasmi na kuomboleza vifo vya watu 39 katika mashambulio ya kujitoa mhanga katika vituo vyake viwili vya treni mjini Moscow siku ya Jumatatu, Rais Dmitry Medvedev amewataka maafisa wa serikali kutunga sheria mpya kupambana na ugaidi.
Ametamka hayo huku Warusi wakiitenga siku ya Jumanne katika kuomboleza.
Warusi wamekuwa wakiwasha mishumaa na kuwacha maua mahali ambako milipuko hiyo miwili ilitokea.
Magazeti ya Urusi yamekuwa yakiilaumu serikali kwa kukosa kuzingatia kikamilifu suala la usalama kwa jumla.

Wazimbabwe 'washinda' Afrika Kusini

Mkulima atathmini uharibifu wa nyumba yake, Harare
Serikali ya Afrika Kusini imekabidhi umiliki wa nyaraka za nyumba moja ya Cape Town inayomilikiwa na serikali ya Zimbabwe kwa baadhi ya wakulima wa Zimbabwe.
Wakulima wa kizungu wanadai fidia kutokana na kunyang'anywa ardhi yao.
Serikali imepewa miezi miwili tu itoe fedha kwa ajili ya gharama za kisheria ilizolipa katika madai yao ya kutaka fidia la sivyo nyumba itauzwa.
Wiki iliyopita, mahakama ya Afrika Kusini ilikubaliana na uamuzi wa mahakama ya jimbo kwamba unyang'anyi wa ardhi kwa nguvu ni kinyume cha sheria.
Uamuzi huo umewapa fursa wakulima waliopoteza ardhi zao kuomba fidia katika mahakama za Afrika Kusini.
Mfanyakazi ya ndani anayedaiwa kuwanga akiwa katika kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Ubungu (UBT) tayari kusafirishwa kurejeshwa kwao Morogoro baada ya tuhuma hizo za kuwangaAbambwa na ndumba kibao na ungo

Walowezi waliotimuliwa wataka mali ya Zimbabwe.


  
Kundi moja la walowezi wa Kizungu ambao walipokonywa ardhi yao na serikali ya Zimbabwe, limewasilisha kesi mahakamani, kutaka kumiliki mali ya serikali ya Zimbabwe ilioko Afrika Kusini.
Wakulima hao wanataka kumiliki ardhi na majengo ya serikali ya Zimbabwe, mjini Cape Town inayokisiwa kugharimu mamilioni ya dola, kama fidia ya kupoteza mashamba yao nchini Zimbabwe.
Uamuzi wao wa kwenda mahakamani, unafuatia ule uliotolewa na mahakama kuu nchini Afrika Kusini, kuwa hatua ya rais Robert Mugabe ya kuwapokonya walowezi hao mashamba ilikiuka sheria.
Uamuzi kama huo pia ulitolewa na kamati ya upatanishi ya nchi wanachama wa muungano wa maendeleo Kusini mwa Afrika SADC.

Rais Bashir aonya wapinzani wake


  
Saa chache kabla ya mkutano wa viongozi wa upinzani nchini Sudan, ambapo wanatarajiwa kutangaza kuwa wanataka uchaguzi uhairishwe, Rais Omar al Bashir ameonya ikiwa watasusia uchaguzi hataruhusu kura ya moani kuhusu kujitawala kwa Sudan Kusini ifanyike mwaka 2011.
Rais Bashir ambaye amekuwa akitoa matamishi makali wiki chache kabla ya uchaguzi huo amenukuliwa na vyombo vya habari nchini humo, akitoa onyo hilo wakati wa kampeni mjini Khartoum.
Chama chake cha National Congress Party ( NCP) kinasisitiza kuwa uchaguzi lazima ufanyike Aprili 11.
Lakini vyama vya upinzani kikiwemo kile cha Sudan's People Liberation Movement (SPLM), kinachotawala kusini mwa nchi hiyo, vinataka shughuli hiyo ihairishwe.
Viongozi wa vyama hivyo wanasema hawaamini kuwa uchaguzi huo utakuwa huru na wa haki.
Kundi la waangalizi kutoka shirika linaloongozwa na rais wa zamani wa Marekani, Jimmy Carter, limekiri kuna matatizo mengi ya utaratibu wa kuandaa uchaguzi huo na wanaunga mkono ucheleweshwe.
Uchaguzi huo unafanyika kulingana na makubaliano ya amani yaliotiwa saini na utawala wa Khartoum na waliokuwa waasi wa SPLA mwaka wa 2005.

Lavrov atoa wito wa ushirikiano dhidi ya magaidi

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergei Larvov, amesema mashambulio ya kujitoa mhanga mjini Moscow hapo jana yameonyesha haja ya kuwepo kwa ushirikiano zaidi wa kimataifa ili kuzuia mashambulio kama hayo.
Akiongea katika mkutano wa mataifa nane tajiri duniani G-8, Bwana Lavrov ametoa wito kwa viongozi wa kimataifa kujitolea kupambana na mitandao ya magaidi duniani.
Naye Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton, amesema mashambulizi hayo ya Moscow, yameonyesha kuwa dunia inakabiliwa na adui mmoja.
Takribani watu thelathini na wanane waliuawa, wakati wanawake wawili walipolipua mabomu waliokuwa nayo karibu na treni mjini moscow, jana asubuhi.
Maafisa wa serikali wamelaumu makundi ya Waislamu Kaskazini mwa nchi hiyo kwa kutekeleza mashambulio hayo. Waasi wa maeneo hayo wamekuwa wakipamabana na vikosi vya usalama wakitaka kujitenga na Urusi. Serikali ya nchi hiyo imeapa kuwasaka na kuwaangamiza waliotekeleza mashambulio hayo
 

Monday, March 29, 2010

Ni Sir Alex Ferguson au Carlo Ancelotti nani kuibuka kidume jumamosi April 3

Carlo Ancelotti, the Chelsea coach, looks on before the pre-season friendly match between Reading and Chelsea at the Madejski Stadium on August 1, 2009 in Reading, England.
Carlo Ancelotti
 Manchester United Manager Sir Alex Ferguson laughs prior to the Barclays Premier League match between Bolton Wanderers and Manchester United at the Reebok Stadium on March 27, 2010 in Bolton, England.
Sir Alex Ferguson

Ricky Martin Comes Out of the Closet


The singer posted a lengthy note on his web site today, with a last line that read: "I am a fortunate homosexual man. I am very blessed to be who I am."

Chris Brown Can't Find a Birthday Party Venue

Chris Brown, Ben J And Legacy And The New Boyz Perform At The Avalon
Sources say he's having a bit of trouble finding a place to hold his 21st birthday party because most joints are worried they'll upset Rihanna if they do so. Ouch

Carrie Underwood Talks Wedding Details

Carrie Underwood Talks Wedding Details
Carrie and her hockey player fiance haven't had much time to plan their big day, but they know this much: There will be cupcakes and much merry-making!

Huwezi amini lakini haya maji...hata nikikwambia ni ya Toilet usishtuke,je wazazi wa watoto hawa wako wapi?????
Image
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua gwaride wakati alipopokelewa rasmi kwenye viwanja vya Ikulu ya Hanoi kuanza ziara ya kikazi nchini Vietnam, jana. Kushoto ni Waziri Mkuu wa Vietnam Nguyen Tan Dung. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Wasomali wapinga vitendo vya Shabab


Mamiya ya wakaazi wa mji wa Mogadishu wamefanya maandamano dhidi ya kundi la Al Shabab. Waandamanaji hao, wengi wanawake na watoto walivaa vitambaa na nguo nyeupe huku wakiwa na mabango yanayounga mkono serikali ya mpito ambayo inamiliki wilaya chache za mji.
Waandamanaji wamesema wanapinga kitendo cha kunajisi makaburi kilichofanywa na kundi la Al Qaeda pamoja na kuleta mamluki wapiganaji wa kigeni.
Mohyadin Hassan Afrah, aliyesaidia kuandaa maandamano amesema kuwa watu walikasirishwa na kitendo cha Al Shabab kuharibu makaburi ya viongozi wa madhehebu ya sufi.
Kundi la Al-Shabab linafuata imani kali ijulikanayo kama Wahabiya ya Saudi Arabia badala ya Sufi inayofuatwa na Wasomali wengi.
Halikadhalika maandamano hayo yanapinga kutumiwa kwa wapiganaji wa kigeni kwenye kundi hilo.
Mwandishi wetu anasema kuwa kuna wapiganaji kutoka Pakistan, Yemen na nchi za Afrika ya kaskazini waliomo kwenye kundi la Al Shabab

Stars na Maryland United


Maryland United

Stars United


Mechi inayosubiliwa kwa hamu kati ya Stars na Maryland United itakayochezwa Dc kweye viwanja vilivyopo 18031 central park circle,boyds,md 20841 tarehe 3 april jumamosi saa kumi jioni(4pm)



Hii mechi itakua ya kwanza msimu huu na ni kati ya mechi za maandalizi na safari ya Stars Sweden mwezi july baada ya mashindano ya kombe la dunia kwisha,tunaomba mashabiki wa Stars kufika kwa wingi kuishangilia Stars

Wachezaji wa Stars wanaotarajiwa kuja ni Michael Mngodo(OH),Aritaf(TX),Amoor,Rahim,Francis Makala,Salum Salum(MA),Ebra Nyangaly(NY),Tif(NJ),Simon Marko,Omari Guy,Denis Geofrey,Inno Geofrey,Shabani Mwampambe,Hamfrey Owen(NC),Hadji Helper,Juma,Edgar Kisoka(ATL),Lemy Mhando,Adam Zimbwe Tenga,Adam Jongo,Aristot Maruma,David Mboss,Evans Shangalai,Rasheed Beach Boy,Gilles,Charles(DC) na Godfrey Oswald(Minnesota),wachezaji Libe,Yahaya,Vicent na Elvis wao wataichezea Maryland United

Mechi nyingine ya Stars itafanyika Boston april 24 dhidi ya Zambia na Wazambia wamepania sana mechi hiyo na wanatuma muakilishi wao kuja Dc kuangalia mechi ya Stars na Maryland united.unaweza kuwatembelea Wazambia kwenye tozuti yao http://nezane.org/soccer-tournament.html ujionee mwenyewe jinsi gani walivyopania mechi hiyo.

Hii timu ya Zambia inaundwa na wachezaji wa Zambia wa Marekani nzima na kunabaadhi walishawahi kuchezea timu yao ya Taifa miaka ya hivi karibuni.Tunaomba washabiki wa Massachusetts wajitokeze kwa wingi baada ya mechi hiyo jioni wazambia watakua na pati yao ya ubwete

Ebra akijianda na mechi ya Stars dhidi ya Md united

Celebrity na Ushabiki wa Michezo


Jack Nicholson mcheza sinema na shabiki # moja wa Los Angeles Lakers akishangilia timu yake ilipocheza na Orlando Magic

Jay-Z akiangalia mechi ya NBA Preseason iliyochezewa ulaya kati ya New Jersey na Miami Heat,mjini London,Uingereza

Mkurugenzi Spike Lee akitoka kwenye kiti chake kuepuka kugongana na mchezaji wa LA LakersTrevor Ariza kwenye mechi ya LA Lakers na New York Knicks

Mcheza sinema Matthew McConaughey akiishangilia Texas Longhorns walipoibamiza Ohio State Buckeys

Enrique Iglesias na Anna Koumikova wakiangalia semifainali ya Tennis aliyocheza Serena Williams kwenye viwanja vya Crandon Park Tennis Center

Ben Affeck na Jennifer Gamer wakiwa uwanjani kwenye mechi ya Baseball kati ya Red Sox na St. Louis Cardinals iliyochezewa Fenway Park,Boston,Massachusetts

Kate Hudson akiangalia New York Yankees wakicheza na Los Angeles mechi ya Baseball

Will Ferrel,mcheza sinema,akiangalia mechi ya Tennis kati ya Serena Williams na Maria Jose Martinez Sanchez