Advertisements

Saturday, April 30, 2011

Deseree Holy Communion & Danita's Baptism

Juu na chini ni Deseree(shoto) akiwa na wenzake kwenye kupata komunio leo jumamosi Glyndon,Maryland
Deseree akipata komunio yake kwa mara ya kwanza
Deseree akiwa na baba na mama baada ya kupata komunio yake ya kwanza na aliyebebwa na mama ni mdogo wa Deseree,Danita ambae nae amebatizwa leo Jumamosi April 30,2011
Juu na chini ni katika ubatizo wa Danita kwenye tendo la kuwasha mshumaa
Deseree na ndugu na marafiki zake wakipata pichaa ya kumbukumbu
Familia ya Deseree ndugu na jamaa wakipata U-kodak moment
Baba wa ubatizo mkuu wa mkoa Columbus OH,Abraham akiwa na mama mwenye nyumba wake na kadogoo wao wakati wakiwa kanisani
Deseree akiwa na Baba yake wakati wakiwa kanisani.
Kwa picha zaidi Bofya Read More

Friday, April 29, 2011

LOOK OF THE DAY

Juiceteefa(Commando Yosso) Leo ni siku yake ya kuzaliwa,May today be filled with sunshine and smiles, laughter and love,HAPPY BIRTHDAY,Not just a year older, but a year better.

NIMEKUWA MPWEKE - YOUNG JULIE - BONGO FLAVA MPYA 2011 INAKUJA



HELLO FRIENDS AND JULIE'S FANS
 
THE FOLLOWING THE SONG HIGHLIGHT  WHICH WILL BE CARRIED ON THE ALBUM. LISTEN HOW THE INSTRUMENTAL AND HOOK WILL BE. EXPECT LOVELY, TENDER AND ROMANTIC VERSES WHEN THE TRACK IS DONE.

Anayeua wanawake Dar es Salaam ashitukiwa

WAKATI hofu ya matukio ya kuuawa kwa wanawake jijini Dar es Salaam ikitanda, jeshi la polisi limepokea taarifa kuhusiana na mtu anayedaiwa kuhusika na matukio hayo yanayofanyika katika nyumba za kulala wageni. 

Hayo yamethibitishwa na Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova. 

Kamanda Kova alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa polisi imepata taarifa kuhusiana na mwanaume mweupe anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30, anayependelea kuvaa suruali aina ya Jeans, fulana nyeupe, raba na kofia kwamba ndiye mhusika wa matukio hayo ya mauaji. 

Bafana Bafana kucheza na Stars May 14,2011

iol spt apr29 Bafana
Bafana Bafana itacheza mechi ya kimataifa ya kirafiki na Tanzania(Taifa Stars) mjini Dar May 14,2011,Chama cha mpira a miguu cha Afrika ya kusini(SAFA) kimethibitisha kuwepo kwa mchezo huo.

Mwenyekiti wa SAFA Pinky Lehoko,amesema kimsingi makubaliano ya kuwepo kwa mechi hiyo yameishafikiwa,na chama cha mpira wa miguu Duniani (FIFA)wameishaiweka mechi hiyo kwenye ratiba.

Timu ya Bafana Bafana ni ya 39 kwa ubora wa mpira wa miguu Duniani na Taifa Stars ni ya 123.

Kocha wa Bafana Bafana Pitso Mosimane anatarajia kutangaza kikosi chake wiki ijayo,kikosi hiki hakitawajumuisha wachezaji wa timu ya Orlando Pirates kwa sababu watakua wanacheza nusu fainali ya kombe la Nedbank wiki hiyo hiyo ya mechi ya Stars na Bafana Bafana.

Mechi hii itakuwa ya mwisho kwa Bafana Bafana ya kujipima nguvu kabla ya timu haijaelekea Misri June 3,2011 kucheza mechi ya kundi G 2012 ya Africa Cup of Nations Qualifier dhidi ya Misri.

Afrika Kusini ndio inayoongoza kundi hiliokwa kufikisha  pointi saba kwa kucheza mechi tatu, kushinda mechi mbili na kutoka sare moja.


Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohammed Shein (kushoto) akilakiwa na Rais wa Uturuki, Abdullah Gul baada ya kuwasili mjini Ankara, nchini humo kwa mwaliko wa rais huyo. (Na Mpigapicha wetu)

Picha iliyochukua tuzo wiki hii

Pichani ni Baba na Mama U wakionyesha malavi davi

Obama atoa cheti chake cha kuzaliwa-VOA

Ni hatua iliyofuatia shutuma zisizokwisha kutoka kwa baadhi ya wapinzani wanaodai kuwa hakuzaliwa katika ardhi ya Marekani
Ikulu ya Marekani Jumatano imetoa hadharani cheti za kuzaliwa cha rais Barack Obama ili kumaliza ubishi unaoletwa na baadhi ya wapinzani kuwa hakuzaliwa nchini Marekani.
Cheti hicho kamili kinaonyesha kuwa Obama alizaliwa Hawaii August 4, 1961 kwa mama Mmarekani Ann Dunham Stanley na baba Mkenya Barack Hussein Obama.

The Royal Wedding Guest List-Zimbio

Kate+Middleton in Prince William And Kate Middleton Visit University Of St Andrews
Prince William and Kate Middleton smile as they visit the University of St Andrews on February 25, 2011 in St Andrews, Scotland. The couple returned to the university where they first met to launch a fundraising campaign for a new GBP 13 million scholarship and students support. The couple will marry in a much anticipated ceremony at Westminster Abbey on April 29th. (Getty Images)more pics »'It's the ticket of the century...thus far. 1,900 people were invited to the royal wedding, and we have a list of the guests you really care about -- and maybe some you don't. But we promise, we'll keep it to celebs and athletes.

The Return Of Memorial Weekend Bashment,COLUMBUS,OH

Si wanawake tu, hata wanaume nao huchezewa na kuachwa!-2

SIKUKUU zimeisha sasa kazi tu! Nimeona hiyo ndiyo salamu nzuri na bora zaidi katika kuhamasishana kufanya kazi. Mimi nipo sawa kwa uwezo wa aliye juu, anayenipa pumzi ya uhai bure.

Mada inayoendelea hapa kwenye Let’s Talk About Love ni namna gani wanaume nao wanavyochezewa na kuachwa na wenzi wao wakiwa na mateso makubwa. Hii ni dhana ambayo kwa baadhi ya rafiki zangu inakuwa ngumu kidogo kuingia akilini mwao.

Kama hakuridhishi mueleze, usitoke nje ya ndoa-GPL

NITAKUWA si muungwana kwa kutotanguliza salamu, ni matumaini yangu wote mu wazima wa afya njema. Tunaendelea kukumbushana mambo muhimu katika mahaba ili ufurahie mapenzi kila siku.
Nimepata maswali mengi juu ya matatizo ndani ya ndoa au ndani ya uhusiano. Imeonyesha pande zote zikifikisha lawama zao huku wakiwa tayari wamekwisha tafuta tiba mbadala kabla ya swali.

Kodi yakwamisha matrekta ya Suma-JKT bandarini

Makontena 364 yenye matrekta ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa nchini (Suma-JKT), yamekwama bandarini kutokana na kudaiwa kodi mbalimbali, ikiwamo ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Hali hiyo inadaiwa kusababisha kukwamisha lengo la matrekta hayo kuwafikia wakulima kabla ya msimu.

Wanafunzi 1,200 Udom watimuliwa

Wanafunzi wa shahada ya kwanza 1,200 wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), katika Chuo cha Sayansi, Mawasiliano na Elimu Angavu, wamesimamishwa masomo kwa muda usiojulikana na kutakiwa kuondoka chuoni hapo kwa kile kilichoelezwa wamevunja kanuni za chuo na hivyo kutishia amani.
Akizungumza na NIPASHE, Kaimu Makamu Mkuu wa Udom, Profesa Ludovick Kinabo, alisema wanafunzi hao walikataa kuingia madarasani hata pale uongozi ulipowataka kufanya hivyo mara kadhaa.
Alisema kuwa kamati ya utendaji ya chuo itakutana Jumatatu wiki ijayo kwa ajili ya kujadili jambo hilo.

Raza awashukia wanaokataa Muungano

Aliyekuwa Mshauri wa Rais Zanzibar, Mohammed Raza, amesema asiyetaka Muungano sio mwana halali wa Zanzibar, kwa vile umesaidia kujenga umoja wa kitaifa na udugu kati ya wananchi wa Zanzibar na Tanzania Bara.
Alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari, mjini Zanzibar jana. “Asiyetaka Muungano sio mwana halali. Na bahati mbaya wanaokataa Muungano hawafahamu faida ya kuwa na umoja,” alisema Raza.

JA RULE 'DISAPPOINTED' WITH PRISON SENTENCE-The Boombox

Matt Jelonek, Getty Images
As Ja Rule prepares to begin his prison sentence in June, the Queens native is revealing that he is saddened by the turn of events that will land him behind bars for the next two years. 

In an in-depth interview with MTV's RapFix
, Rule opened up about his regret. "I'm disappointed," he explained. "I'm mad at myself."

For Rule, the hardest part about going to prison will be leaving his family behind. The father of three will begin and end his sentence missing his teenage daughter Brittany's last years in high school. "My daughter, she's 15 right now," he continued. "These are her last couple of years. She's about to graduate from high school, and she's going to college. She needs her father. My boys really need me right now too, as well as my wife. They need Daddy, and Daddy f---ed up."

Rule's pending imprisonment is the first time that the 35-year-old has been incarcerated. As previously reported, the former Murder Inc. artist pleaded guilty to weapons possession charges, stemming from a 2007 arrest. The rapper was pulled over following a show at New York City's Beacon Theater, when police discovered a loaded semiautomatic in his vehicle. His sentencing has been scheduled for June 8.

The 'Always on Time' creator is set to release two albums: 'Pain is Love 2' and 'Renaissance Project.' Both projects are scheduled to be released on June 7, one day before his prison sentence commences.

Babu arejea Samunge, tiba kuanza tena leo

Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapila
Mussa Juma, Samunge
MCHUNGAJI Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapila, maarufu kwa jina la 'Babu,' amerejea Samunge jana na leo anatarajiwa kuendelea kutoa tiba kwa wagonjwa waliokuwa wakimsubiri kwa siku tatu mfululizo.
Mchungaji Mwasapila aliondoka Jumanne jioni na jana alirejea kutoka wilayani Babati, mkoani Manyara alikohudhuria mazishi ya mtoto wake Jackson (43), akiwa anaongozwa na maofisa usalama na polisi.
Mchungaji Mwasapila, aliondoka kijijini Samunge saa 12:20 jioni katika gari la Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro ambalo lilibeba pia maofisa hao wa usalama, polisi na wasaidizi wake.  Awali, kabla ya kuondoka Samunge, watu mbalimbali walikuwa wamejitolea kumsafirisha mchungaji huyo, lakini walizuiwa kutokana na sababu za kiusalama.

Tonight April 29,2011 @ Millenium,Free To Get In B 4 Midnight

International Friday
plus
Zimbambwean Night
Fri April 29,2011
karibuni

MAMA BISHANGA AMEREMETA

Picha Juu ni Christina Innocent akiwa na mumewe Mr Marolen ambae ni mfanya biashara Johannesburg na    ambae asilia amatokea Limpopo South Africa, Christina na Marolen walifunga  ndoa tarehe 5 march 2011, katika kanisa la st peters Oysterbay, na reception ilifanyikia  Peacock hotel Dar es slaam.
Picha chini Bwana na Bibi Harusi wakipata picha ya pamoja na familia nje ya kanisa la St Peter,

Thursday, April 28, 2011

Kheri Yahaya anawataarifu Mazoezi kwa Watoto J'2 May 1,2011 4:30pm


KOCHA ANATOA TARIFA YA MAZOWEZI KWA KUJITOLEA KUFUNDISHA WA TOTO KILA JUMAPILI KATIKA KIPINDI HIKI CHA SUMMER.

kids make sure you bring soccer ball
soccer boot
shin guards
soccer sock
soccer T-shirt
soccer short


MD DC VA all East African Kids soccer camp I will start this weekend free 4 1hr we looking forward to see more kids thank you last chance ppls kids stop play video game we start age 6yrs to 15yrs we want to make very good team
Address
9701 Meadowbrook Lane,
Chevy Chase,MD

Karibu


CHAMA CHA MAPINDUZI

[Chama Cha Mapinduzi]
Tawi  la Marekani
April 28, 2011
TANGAZO LA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA TAWI
Ndugu Wanachama,
SIKU YA MWISHO YA KUCHUKUA FOMU ZA UONGOZI NI 
JUMAPILI, MAY 8, 2011.
TAREHE YA UCHAGUZI NI JUMAPILI MAY 22, 2011.  KATIKA UKUMBI WA 2200 TANGLEWILDE HOUSTON, TX. 77063, KUANZIA SAA 8 MCHANA MPAKA SAA 4 USIKU.
Kwa kukumbushia tu nafasi zitakazogombaniwa ni hizi zifuatazo;
·        Mwenyekiti wa Tawi na,
·        Wajumbe kumi wa Halmashauri kuu ya Tawi.
Kwa wale wanachama wanaoishi mbali na mji wa Houston,TX. Kamati ya uchaguzi inafanya utaratibu wa kuwawezesha  kupiga kura mapema (early voting), mara tu majina ya wagombea wote yatakapojulikana.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na kamati ya uchaguzi katika ccmmarekani@gmail.com  au ingia  http://ccmmarekani.blogspot.com
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI,
Abdallah Nyangasa
Kaimu Katibu Mkuu,
CCM-Marekani.

TAARIFA KWA WANA NEW YORK METRO.

NDUGU WANA NEW YORK METRO,
 Jina langu naitwa Hajji Khamis,mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio maeneo ya New York,New Jersey,Pennsylvania na Connecticut.
 Kwa kuanza nnawaomba wana New York metro wenzangu tujitokeze kwa wingi ili tuweze kuchagua viongozi watakaotuwakilisha katika kipindi hiki.Pia ningependa kuwashawishi wale wote ambao hawakujisajili na jumuiya yetu wafanye hivyo kupitia kwa wahusika na wale ambao hawatopata nafasi waje kwenye uwanja wa uchaguzi wataruhusiwa kujisajili hapo na wataweza kupiga kura na kuchagua viongozi wao.Anuani ya mahali tafadhali ingia kwenye website ya jumuiya(www.nytanzaniancommunity.org).Tafadhali tufike saa nane kamili bila kuchelewa.

  KAMA MGOMBEA WA NAFASI YA MWENYEKITI WA MWANZO WA JUMUIYA YETU,
  1) Lengo langu kuu ni kuwaunganisha wana New York Metro bila kujali dini,kabila ama jinsia.Kuleta mapenzi baina yetu na kujenga moyo wa kuaminiana.
  2) Kubuni programu  zitakazotuwezesha kuwapatia watoto wetu scholarship ili waweze kuleta ushindani mashuleni.Watoto wetu ndio future yetu.
  3) Kubuni njia zitakazosaidia wanacommunity kuingia kwenye ulimwengu wa ujasiriamali na kadhalika.

 Wana New York kwenda mbele tunahitaji umoja na kuwa na umoja imara tunahitaji viongozi imara wenye moyo wa kujitolea kusaidia wanacommunity.Historia yangu inaonyesha ushiriki wangu na uwezo wangu kusikiliza,kuwasiliana na kuwaunganisha wanajumuiya.
  Jumuiya yetu hii ni muendelezo wa jumuiya tuliyoianzisha mwaka jana chini ya uongozi wangu wa muda.Katika kuhakikisha tunamshirikisha kila Mtanzania anaeishi maeneo haya ya Metro,tuliunda kamati iliyohakiki jumuiya ile na kwa kuafikiana tumeafiki wakati muafaka wa kuchagua viongozi wa jumuiya yetu.
  Uongozi wangu wa muda uliweza kuendeleza mahusiano mazuri na balozi zetu mbili za Washington na New York yaliyopelekea kufanikisha mengi ukiwemo ujio wa Muheshimiwa Waziri Mkuu.Uongozi wangu ulimvutia waziri mkuu kiasi cha kuamua kutufanyia fund raise ya zaidi ya dola $10,000.00.Pia tulishirikiana kwa karibu katika misiba na mengineyo.
  Wana New York Metro,naomba kura zenu ili niweze kumalizia kile nilichokianza kwa manufaa ya wote.Tujumuike pamoja ili tujenge jumuiya iliyo imara.Tujumuike kuwaleta wana New York Pamoja.

 UMOJA NI NGUVU
MGOMBEA UENYEKITI
 HAJJI KHAMIS.

Polisi aliyelala nje mwezi na familia apata nyumba


Image
Vijana wakazi wa eneo la Polisi Ufundi barabara ya Kilwa Dar es Salaam wakisaidia kuweka vyombo ndani ya nyumba ambayo ilikuwa inakaliwa na mtu asiyekuwa askari baada ya gazeti hili kuandika habari hizo Aprili 27. Nyumba hiyo sasa amepewa askari mhusika. (Picha na Yusuf Badi).

HATIMAYE askari Polisi aliyekuwa akilala nje na familia yake kwa mwezi mmoja baada ya kuzuiwa kuingia ndani ya nyumba aliyopewa, jijini Dar es Salaam amekabidhiwa nyumba hiyo chini ya usimamizi wa Mkuu wa Polisi wa Kituo cha Kati (OCS), Pili Mande.

HABARILEO limemshuhudia mke wa askari huyo, Sofia Gapile, akiingiza samani zake ndani ya nyumba hiyo, huku samani za aliyekuwa akizuia nyumba hiyo kwa nguvu, mtoto wa Sajini Pascal zikitolewa nje na kuhifadhiwa katika stoo ya nyumba za Polisi eneo hilo. 

Wavulana wafanya kweli 'form six'

UFAULU wa mtihani wa kidato cha sita kwa mwaka huu umepungua kwa asilimia moja ikilinganishwa na mwaka jana. 

Wavulana wameibuka kidedea kwa kushika nafasi zote 10 bora.

Pamoja na hayo, masomo ya Sayansi, Biashara na Hisabati ni miongoni mwa yaliyoongoza kwa kufaulisha wanafunzi wengi ikilinganishwa na Sayansi ya Jamii na Sanaa, huku wanafunzi wengi wakifeli zaidi katika masomo ya lugha za Kiswahili na Kiingereza.
MAISHAMEMA EDUCATION AND TRAINING CENTRE      
Proper knowledge        P.O. BOX 35967,      E-mail:  MAISHAMEMA@GMAIL.Com
          For                     DAR ES SALAAM     Mobile:   0716868425
Genuine Solution                                                             0719268764
                                    Website: http//maishamematanzania.blogspot.com

NAFASI   YA   MAFUNZO   NA  KAZI

Wewe  ni  kijana wa  kike mwenye  umri  wa kati  ya  miaka  18  hadi 35?
Una  elimu  ya  kuanzia  kidato  cha  nne, sita  na  kuendelea?
Unapenda  kufanya  kazi  ya  kuwaelimisha  vijana  wenzako  wa  kike  waliopo  mashuleni, vyuoni  na  magerezani  juu  ya  madhara  ya  vitendo  vya  kisagaji?

Kama jibu  ni  ndio  basi  hii  ni  habari  njema  sana  kwako. Kituo  cha  Elimu, Mafunzo, Utafiti  na  Uimarishaji  Maarifa  cha  MaishaMema  Education &  Training  Center  cha  jijini  Dar  es  salaam  kupitia  katika  mradi  wake  wa “ Sexualitity  Education  &  Awareness  Project  Campaign” ( SEA  Project  Campaign ), kinatangaza  nafasi  hamsini (  50 )  za  mafunzo  na  kazi  kwa  vijana  wa  kike  wa  kitanzania  wenye  sifa  tajwa  hapo  juu   kwa  ajili  ya  kupata  mafunzo  yatakayo  wawezesha  kufanya  kazi  na  kituo  katika  mradi huu.

ADA  YA  MAFUNZO: Mafunzo  yanatolewa  bure  kabisa.
ADA    YA  KUJISAJILI:   Ada  ya  kujisajili  katika  mafunzo  haya  ni  shilingi  Elfu  Thelathini  Tu ( Tshs. 30,000 )  ambayo itajumuisha  gharama  za  kitambulisho  na  T.Shirt..

MUDA  WA  MAFUNZO:
Mafunzo  yatachukua  miezi  miwili. Mwezi  mmoja, mafunzo  ya  darasani  na  mwezi  mmoja  wa  mafunzo  kwa  njia  ya  vitendo (  Field  Trainings )

Baada  ya  mafunzo, wahitimu  watafanya  kazi  na  kituo  katika  mradi  huu.

Mafunzo  yataanza   tarehe  09  MAY  2011. Na  yatakuwa  yakifanyika  katika  shule  ya  sekondari  Perfect  Vision, kuanzia  saa  nane  na  nusu  za  mchana  hadi  saa  kumi  na  mbili  na  nusu  za  jioni.
Mwisho  wa  kujisajili    ni  tarehe  07 MAY  2011.  Endapo  idadi  ya  watu  tunao  wataka  itatimia  kabla  ya  tarehe  07  MAY 2011  tutasitisha  zoezi  la  kusajili..

KUJISAJILI.  Fika  katika  ofisi  zetu  zilizopo  katika  shule  ya  Sekondari  Perfect  Vision, iliyopo  karibu  na  jengo  la  Ubungo  Plaza.


KWA  MAELEZO  ZAIDI.PIGA  0719268764.  AU  O716868425

Tangazo la Ibada Mei Mosi, 2011 Columbus, Ohio

Rais Obama akutana na mwana mfalme wa Abu Dhabi-VOA

UAE na Qatar ni nchi mbili pekee za Mashariki ya Kati zinazosaidia NATO katika hatua zake za kijeshi dhidi ya kanali Moammar Gadhafi
Taarifa ya White House baada ya mazungumzo hayo inaeleza kwamba viongozi hao wawili walijadili masuala mbali mbali kuhusu hali ya Mashariki ya Kati na yalikuwa majadiliano yenye manufaa, lakini haikutoa maelezo zaidi.
Kwa upande wake shirika la habari la Emirates lilitowa maelezo zaidi likiripoti kwamba mazungumzo yalihusu msaada unaotolewa na Umoja wa Nchi za Karabu UAE, kwa NATO katika hatua zake za kijeshi nchini Libya na juhudi za kuzuia kuenea kwa siasa kali.

Malawi na Uingereza 'zatunishiana misuli'-BBC

Uingereza imetoa amri kwa balozi wa Malawi kuondoka nchini humo kufuatia kufukuzwa "kusiko sawa" kwa balozi wa Uingereza nchini Malawi.
Bingu
Rais Mutharika
Balozi wa Uingereza Fergus Cochrane-Dyet alitakiwa kuondoka Malawi baada wa kukaririwa katika waraka uliovuja akisema rais havumilii kukosolewa.

Usiombe ukaoa binti mzuri, aliyesoma lakini asiyejua kupenda!-GPL

Natumaini umzima bukheri wa afya na unaendelea vyema na michakato mbalimbali ya maisha yako. Mimi namshukuru Mungu kwa kunijaalia uzima ambao ndiyo umenifanya leo hii niweze kuwaletea mada nyingine ikiwa ni katika kuwekana sawa juu ya maisha yetu ya kimapenzi.

Mpenzi msomaji wangu, naamini wapo walioshituka kuona kichwa cha habari hicho hapo juu lakini ni ukweli usiofichika ambao leo nimelazimika kuuandika ili wanaume wenzangu wanaotaka kuingia katika maisha ya ndoa wawe makini katika kuchagua wenza sahihi.

Barua za watuhumiwa ufisadi CCM bado kitendawili

Suala la kuwakabidhi barua makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaotuhumiwa ufisadi za kuwaarifu kuondolewa katika uongozi wa chama, limezidi kuwa gumu kwa chama hicho.
Hali hiyo imedhihirika, baada ya sekretarieti mpya iliyoingia madarakani mwezi huu, kuendelea kutupiana mpira juu ya lini kazi hiyo itakamilishwa.

Mshana amrithi Tido Mhando TBC

RAIS Jakaya Kikwete amemteua Clement Mshana kuwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC). 

Rais Kikwete pia amemteua Katibu Mkuu mmoja wa Wizara na naibu makatibu wakuu 10. 

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu iliyotolewa jana na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, George Yambesi, Mshana anachukua nafasi ya Tido Mhando aliyemaliza muda wake wa utumishi kwa mujibu wa mkataba. 

Yambesi alisema, uteuzi huo wa Mshana ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), ulianza Alhamisi.
Image
Gari la Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa, Chita, iliyopo Tarafa ya Mngeta, Kilombero likiwa limenasa katika Kijiji cha Kisegese ambapo barabara yake ya kutoka Ifakara - Mlimba imeharibika vibaya kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua za masika. Hata hivyo gari hilo lilifanikiwa kujinasua na kutoa msaada kwa magari mengine yaliyokuwa yamekwama eneo hilo kwa zaidi ya siku mbili. (Picha na John Nditi).

Babu aenda msibani chini ya ulinzi

Mchungaji Ambilikile Mwasapila (alishika koti),akisubili kupanda gari ili aondoka katika kijiji cha Samunge, mkoani Arusha juzi, kwenda Babati kuhudhuria mazishi ya mtoto wake,Jackson Mwasapila aliyefariki katika Hospitali ya wilaya ya Babati. Picha na Mussa Juma
Mussa Juma, Samunge
MCHUNGAJI Ambilikile Mwasapila anayetoa tiba ya magonjwa sugu huko Samunge Loliondo, juzi jioni aliondoka hapa kwenda Babati, Manyara kuhudhuria mazishi ya mtoto wake huku safari yake hiyo ikiratibiwa na Serikali na akipewa ulinzi mkali wa maofisa usalama na polisi.

Aliondoka Samunge saa 12:20 jioni na gari la Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro akiwa na maofisa hao wa usalama, polisi na wasaidizi wake. 
Kabla ya kuondoka Samunge, watu mbalimbali walikuwa wamejitolea kumpatia usafiri mchungaji huyo lakini walizuiwa kutokana na sababu za kiusalama.

Chenge: Sijui kama mimi ni gamba CCM

MBUNGE wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge amesema anasubiri taratibu za Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuona kama atapewa barua ya kumtaka ajivue nafasi zake za uongozi kwani hadi hivi sasa hajui kitu hicho.Kauli hiyo ya kwanza ya Chenge inakuja kipindi ambacho Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amekuwa akitangaza kwa nguvu mpango mkakati wa chama hicho kujivua gamba.

Makada wa chama hicho wanaotakiwa kupima nafasi zao na uzito wa tuhuma zinazowakabili ni wale wanaohusishwa na kashfa mbalimbali zikiwamo za Richmond, Kagoda na wizi wa EPA.

Wednesday, April 27, 2011

MAMA WA MITINDO KUTOKA TANZANIA ASIA IDAROUS KHAMSIN KUUNGANA NA WATANZANIA WA SEATTLE USA KUSHEREHEKEA MIAKA 50 YA MUUNGANO KWA KUONYESHA MITINDO YA KITANZANIA SIKU YA JUMAMOSI TAREHE 30 APRIL 2011.

KAJUMULO FC KWA WA TANZANIA WANAO ISHI USA KWA WATOTO WA KIKE NA KIUME

OK KAMA KUNA WATOTO WA KITANZANIA WANAO TAKA KUCHEZA MPIRA KWENYE CLUB YA MPIRA YA KAJUMULO FC  WANAWEZA KUJIUNGA WATOTO WAWE WENYE MIAKA 10/11/12/13/14/15/16 KILA TIMU TUNATOA NAFASI MBILI KWA WAZAZI WA SIO NA KIPATO CHA KUTOSHA. NA NITAJITOLEA KAMA NI WATOTO WA KITANZANIA NITATOA NAFASI BULE KILA TIMU WATOTO WA 4 BURE .THANKS ONE LOVE IS LAW.

Umewahi kujiuliza, naye anakupenda?

SINA shaka marafiki zangu mtakuwa wazima wa afya njema na sasa mnaendelea na majukumu yenu kama kawaida baada ya kumaliza mapumziko ya siku tano. Tangu Ijumaa hadi jana ilikuwa ni Sikukuu mfululizo!

Ni jambo la kumshukuru Mungu kama sherehe zimemalizika salama bila kukutana na balaa la aina yoyote. Kilichobaki kwa sasa ni kuchapa kazi kwa nguvu ili kusukuma mbele gurudumu la maisha.
Leo nimekuandalia mada nzuri ambayo nina imani baada ya kumaliza kuisoma utakuwa na mabadiliko makubwa katika maisha yako ya kimapenzi.

UNAUKUMBUKA MSHUMAA HUU???

JIM JONES ARRAIGNED IN NYC FOR SUSPENDED LICENSE ARREST-The Boombox

jim jones perfect day videoGetty Images
Jim Jones doesn't seem to learn from his mistakes. Capo had another date with a judge today (April 26). The Dipset rapperwas arraigned in a New York City courtroom for driving on a suspended license charge.

Jones was arrested on March 30 after cops pulled over his Bentley and found him in possession of the bunk driver's license due to an unpaid ticket. He was cuffed, booked and released the same day. Jones, known to have a fiery attitude, actually praised his arresting police officers following the incident. "They showed me total respect," he told the New York Daily News at the time. "Every officer in there is a gentleman."

This isn't the first time unpaid tickets have gotten Jones, born Joseph Guillermo Jones II, in trouble. In 2009, Capo was booked for an outstanding warrant stemming from an unpaid parking ticket. At the time he even tweeted, "I decide to drive by myself ... let's see how this plays out ... the funny part was watching them have to count all the money in my pocket lol I must say they were very cool ... And it was a punk ass warrant from 2005 for 120 dollars...Make sure you pay old tickets."

According to the Associated Press, lawyers for Jones allege the rapper "did not realize" he had an unpaid ticket at the time of his March arrest.

Jones released his fifth solo album 'Capo' on April 5. The album's first single, the pop-rock infused 'Perfect Day,' was followed-up by the bass-heavy, Aaron LaCrate-produced 'Everybody Jones' -- both a huge departure from Jones' usual solo work and lab time with Dipset.

AngloGold, African Barrick in ‘Advanced’ Talks on Tax Refunds in Tanzania


AngloGold Ashanti Ltd. (ANG)African Barrick Gold Ltd. (ABG) and other miners of the precious metal are in “advanced” talks with Tanzania’s government about a $273.9 million tax refund, the Chamber of Minerals and Energy said.
Tanzanian tax policy for the mining industry provides for a refund of duties on fuel used to generate electricity to power gold mines, as well as value-added tax, or VAT. Miners are claiming about 60 percent of the total amount in refundable fuel duties and 40 percent from VAT, said Godvictor Lyimo, chairman of the finance committee at the chamber.

Mafisadi CCM waandaa mamilioni kujisafisha

Wadaiwa kuandaa vijana kupinga hatua dhidi yao

Na John Daniel

KUNDI la mafisadi wanaokabiliwa na hatihati ya kuvuliwa uongozi na pengine uanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamebuni mbinu mpya
kujihami kwa kutumia haramu kwa kuandaa vijana kufanya maandamano kumpinga Rais Jakaya Kikwete na chama chake.

Kundi hilo linapinga vikali uamuzi wa CCM kupitia Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), kuwapa muda wa kujiengua wenyewe kabla ya kufukuzwa baada ya siku 90.

Azam yamuweka sokoni Ngassa

Uongozi wa timu ya soka ya Azam FC ya jijini Dar es Salaam umesema kuwa uko tayari kumuuza mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu uliomalizika, Mrisho Ngassa lakini ukitoa angalizo kuwa klabu yoyote inayomtaka ijiandae kuvunja 'benki' ili kumtwaa.
Ngassa amekuwa akitajwa na baadhi ya wadau wa Yanga kwamba huenda akarejea katika klabu yake hiyo ya zamani na kwamba tayari Kamati ya Usajili ya Wanajangwani inatarajia kufanya harambee maalumu kusaka fedha zaidi za usajili.

Mafisadi wanamiliki mikoa, wilaya, kata

Mbunge wa Kahama, James Lembeli, ameshauri wimbi la kujivua gamba ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) liendelee hadi ngazi ya mkoa, wilaya, kata na matawi ambako amedai kumejaa mawakala wa mafisadi.
Alisema kamati ya siasa ya mkoa wa Shinganga inayoongozwa na Hamisi Mgeja, nayo inapaswa kujivua gamba kwani imeshindwa kutimiza wajibu wake.